Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Februari 8 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting
itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Prisons itakuwa ikiingia uwanjani ikiwa katika nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 10 mara baada ya kushuka dimbani katika 14 ya ligi hiyo ilhali Ruvu Shooting ikiwa na alama 19.
Katika mchezo uliopita Ruvu Shooting walikwenda sare ya bila mabao dhidi ya Mgambo huku Prisons na wakiambulia sare ya bila mabao dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Mlandizi mkoani Pwani Ruvu Shooting waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Mechi
nyingine nne za ligi hiyo zitachezwa keshokutwa (Februari 9 mwaka huu) kwenye
viwanja mbalimbali. Mgambo Shooting vs Simba (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT vs
Kagera Sugar (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers vs Coastal Union
(Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Mbeya City vs Mtibwa Sugar (Sokoine, Mbeya).
No comments:
Post a Comment