Bingwa wa dunia wa ngumi za uzito wa juu Vladimir Klitschko atatetea
taji lake dhidi ya Alex Leapai mjini Oberhausen , nchini Ujerumani
tarehe 26 Aprili mwaka huu.
Klitschko mwenye umri wa miaka 37, ambaye
anashikilia mikanda ya WBO, WBA na IBF atatetea mataji yake hiyo dhidi
ya raia huyo wa Australia ambaye anapambana kuwania mataji ya kimataifa
kwa mara ya kwanza.
Leapai mwenye umri wa miaka 34, ameshinda mara 30
kati ya mapambano yake 37, akishindwa mara nne na sare mara tatu.
No comments:
Post a Comment