Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic, amedhibitisha ataondoka
timu hiyo mwishoni wa musimu huu huku akidhamiria tangazo hilo
litasitisha uvumi kuhusu hatima yake.
“Nimeamua nitasonga pengine mwisho wa musimu huu,” alisema kwenye taarifa iliyochapishwa katika tovuti rasmi la timu hiyo.
“Huu ndio mwaka wa mwisho wa kandarasi yangu na nimefurahia miaka nane ya ufanisi hapa.”
Ripoti za vyombo vya habari Uingereza zilizua tetesi kuwa kinara
huyo hajawasilishiwa ombi la kuongezewa muda Old Trafford huku Vidic
akisisitiza hataki kuchezea klabu kingine taifa hilo.
“Nataka kujipatia changamoto tofauti na kujaribu kujiboresha miaka
inayofuatia. Sitazamii kuishi Uingereza kwani United ndiyo timu pekee
nilitamani kuchezea hapa na nina bahati kuwa sehemu ya klabu hiki kwa
miaka mingi,” alifafanua.
“Nimepata chaguo kadhaa na nitaona ni wapi kunakofaa kwangu na
jamii yangu kwenda,” mlinda ngome huyo wa Serbia ambaye amehusishwa na
kuhamia magwiji wa Italia, Inter Milan, aliongeza.
Kulingana na kanuni za Bosman, Vidic yuko huru kuzungumza na vilabu nje ya Uingereza.
Vidic aliwasili Old Trafford 2005 kwa dhamani ya pauni milioni saba
za Uingereza kutoka Spartak Moscow na muhula uliopita, aliongoza United
kunyakua taji la kihistoria la 20 kabla ya mwalimu wake wa awali, Sir
Alex Ferguson, kustaafu.
No comments:
Post a Comment