KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 26, 2014

PAMOJA NA KUFUNGWA NA CITY BADO UNITED WALIKUWA KATIKA KIWANGO SAFI

Moyes pichani akiwa katika hali ya kutokujiamini
Manchester City iliendelea kujiimarisha na kuikosesha amani klabu ya Manchester United katika ligi kuu ya premier.
Sio hilo tu bali Man City wanaongeza shinikizo kali kwa Chelsea walio juu kwenye jedwali la ponti katika ligi hiyo.
Man Uinted walipata kichapo cha mbwa cha mabao matatu bila nyumbani Old Trafford.
Edin Dzeko aliingiza mabao mawili katika kila kipindi kwa City hapo jana huku Yaya Toure akizidisha machungu kwa bao la tatu mwishoni mwa mechi bila jibu kutoka kwa Man United.
Sasa vijana hao wa City wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.
Under guard: Walinzi walio katika mavazi rasmi ya jaketi za rangi ya machungwa wakiimarisha ulinzi katika eneo la Stretford End kuhakikisaha hakuna mtu atakae lidhuru bango kubwa pichani lenye maandishi ya THE CHOOSEN ONE.

Moyes alijiamini kabla ya mchezo huo kutokana na matokeo ya kushangaza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Olympiacos pia mchezo dhidi ya West Ham katika ligi ya England.

 
Baada ya mchezo, Moyes alikaririwa akisema kuwa kikosi chake kilikuwa vizuri katika mchezo huo.
 
Amekaririwa akisema 
'Hatukuanza mchezo vizuri lakini kwa kadri mchezo ulivyokuwa ukiendelea tulikuwa kimchezo na mapaka tunafungwa goli la pili tulikuwa tukitafuta nafasi lakini hatukuwa wazuri katika umaliziaji.

'I think we have played a very good side, playing at the sort of level we are aspiring to. We need to come up a couple of levels ourselves because at the moment we are not there.' 


Meneja wa City Manuel Pellegrini yeye alikuwa na haya ya kusema baada ya mchezo

'Tumefunga magoli matatu na tulikuwa na nafasi tatu kama si nne nzuri za kufunga zaidi. Sikumbuki nafasi nyingi za tulianza kwa alama tatu tangu dakika ya kwanza ya mchezo.

'Kwangu ni muhimu kulinda 'clean sheet'.Tulijua tungefunga magoli mengi, tulikuwa tunacheza pamoja na kufanya kazi kwa ukamilifu sehemu zote ushambuliaji na ulinzi

'Ni muhimu wakati wa kuanza msimu kuwa na kikosi unacho kihitaji,unapaswa kucheza michezo mingi ni vema kuwa na washambuliaji wengi, lakini nina furaha juu ya aina ya ulinzi wetu, tuna mizania sawa ya kikosi kwasasa'

No comments:

Post a Comment