Maafisa wa Fifa akiwemo Rais wa chama hicho,Sepp
Blatter na Michel Platini wamehojiwa kuhusu uhalali wa mkataba wa
kuandaa michuano ya Kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 kwa Urusi na
Qatar.
Rais wa Fifa, Blatter na Platini wa shirikisho
la soka barani ulaya Uefa, walishiriki katika mchakato huo mwezi Desemba
mwaka 2010.
Mkuu wa kitengo cha upelelezi ndani ya Fifa anafanya uchunguzi namna ambavyo mchakato huo ulifanyika.
Jumla ya Wajumbe 13 kati ya 24 waliokuwa kwenye kamati wamekuwa wakihojiwa kuhusu sakata hilo.
Baadhi ya walioshiriki kupiga kura wamestaafu
huku wengine wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa halikadhalika
kushinikizwa kuacha kazi baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria ya
Fifa.
Hatua hii haina uhusiano na uchunguzi uliofanywa
na gazeti la Daily Telegraph kuhusu maafisa wa zamani wa Fifa, Mohamed
Bin Hammam na Jack Warner wanaohusishwa na utoaji wa mkataba wa kuhodhi
mashindano ya Kombe la dunia kwa Urusi mwaka 2018 na Qatar mwaka 2022.
Juma hili, imeeelezwa kuwa kuwa kuwa shirika la
upelelezi FBI linachunguza malipo yanayodaiwa kutolewa na Kampuni ya
Bin Hammam kwa Warner na Watoto wake muda mfupi baada ya zoezi la
upigaji kura kukamilika.
No comments:
Post a Comment