Nyota wa kimataifa wa Ghana Kwadwo Asamoah amesisitiza kuwa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana maarufu kama 'Black Stars' kimeunganishwa na kocha Kwesi Appiah.
Tangu kukiongoza kikosi mpaka kutinga kombe la dunia kitu kimemfanya Appiah kujibu tetesi zilizo enea nchini Ghana kuwa FA ya nchi hiyo inataka kumwajiri kocha mgeni kumsaidia kwenye fainali za kombe la dunia.
"Yeye ndiye tuliyekuwa naye wakati wote wa kuwania kufuzu na tuko naye, wachezaji bado wanamuamini" Asamoah ameliambia shirika la utangazaji la nchini England BBC.
"tungekuwa hatumuamini ingekuwa ngumu kwetu na kwake."
"Tunaye yeye sasa hivyo tunawajibu wa kujituma kwa nguvu zetu zote kwa ajili yake na kumuunga mkono"
"Mkiwa wachezaji mnamuunga mkonio mwalimu naye pia mwalimu anapa kujiamini katika kazi yake"
No comments:
Post a Comment