Shirikisho la Kandanda la Afrika (CAF) limethibitisha
kuwa ni mashabiki 5,000 pekee watakaoruhusiwa kuingia kwenye uwanja wa
Tata Rapahel mjini Kinshasa kwa mechi ya Jumapili ya Ligi ya Mabingwa wa
Afrika kati ya AS Vita na wakinzani wao kutoka Misri Zamalek.
Hii inafuatia msongamano uliofuatiwa na msukumano katika uwanja huo ambapo watu kadhaa walifariki.
Watu 15 walifariki na wengine zaidi kujeruhiwa katika mechi katika AS Vita na wapinzani wao TP Mazembe.
Kiwango cha mashabiki wanaotazamiwa kufika
uwanjani kiliafikiwa katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika kundi "A" kati ya
chama cha kandanda katika DRC (FECOFA) na maafisa wa usalama.
Hatua hizo zimechukuliwa ili kuepukana na msongamano katika uwanja huo.
Mashabiri waliojisahili na walio na vyeti sahihi vya uanachama watapewa nafasi ya kwanza kuingia uwanjani.
CAF wamesema kuwa mwanachama wa kamati kuu ya
FECOFA wakiongozwa na Rais wake Constant Omari, wamekagua vifaa katika
uwanja huo ili kuhakikisha kuwa kutakuwepo na usalama.
No comments:
Post a Comment