Hiyo juu ni safariinaendelea kuifuata fainali uwanja wa Parc des Princes dhidi ya Rennes |
KUTOKA jina la Gunners mpaka kuitwa Trotters, jina la utani halijatoa maana ya mpango mzima lakini hiyo si kitu kwa Guingamp.
Klabu hiyo ya nchi Ufaransa maarufu kwa jina la 'wakulima' sasa wanalichukulia jina hilo katika uhalisia na kuwafanya mashabiki wake kuonyesha kuwa kuwa kweli wao ni wakulima.
Kabla ya mchezo wa fainali ya Coupe de France dhidi ya Rennes usiku wa leo, mamia ya mashabiki wa klabu wamekuwa wakielekea katika uwanja wa Parc des Princes kwenye mchezo mchezo huo wa fainali wakitumia vifaa vyao vya kazi kama usafiri wakipanda matrekta.
Hiyo ni kweli, wamesahau treni, ndege na magarimashabiki wa Guingamp wao wakiwa ni wakulima wa kweli waliamua kuishuhudia fainali hiyo kwa kupanda matrekta.
Licha ya safari kuwa ndefu, kwani kwa kutumia magari ya kawiada muda utumikao ni masaa manne na nusu, lakini mashabiki hao wakalazimikia kuchukua tahadhari ya muda wakianza safari mapema.
No comments:
Post a Comment