KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, May 2, 2014

Brendan Rogers: Roberto Martinez anaweza kuisimamisha Manchester City

Hali ya kujiamini: Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers anajiamini kuwa wapinzani wao wa taji Everton watapambana dhidi ya Manchester City

Brendan Rodgers anaamini kuwa Everton itafanya kila iwezalo kuwafunga wapinzani wao wakubwa katika kulifukuzia taji la ligi kuu ya England msimu huu Manchester City wikiendi hii.

Ushindi au sare kwa Toffees utawarejesha Reds katika ahueni na udhibiti wa kuliwania taji hilo na kuimarisha matumaini ya kutwaa ubingwa.

Baadhi ya mashabiki wa Everton wanaonekana kuonyesha kutaka klabu ya kuwasidia majirani zao wa karibu na mitaa ya Stanley Park Manchester City kumaliza vinara katika msimamo wa ligi lakini Rodgers anasisitiza kuwa hana wasiwasi na uadilifu wa meneja Roberto Martinez na wachezaji wake.
Mawazo mchanganyiko: Mashabiki wa Everton wanataka timu yao ipoteze mbele ya Manchester City ili kuwazuia Liverpool kushinda taji.
Akiongea katika mkutano na wanahabari kabla ya mchezo wao utakao pigwa Jumatatu dhidi ya Crystal Palace, Rodgers amesema
'Naamini kutankuwa na mtikisiko mwingine katika kulikimbiza taji.

'Manchester City ina mchezo mgumu. Everton ni klabu kubwa watakuwa wakipambana kupata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kumaliza katika nafasi nne za juu, sisi tutakazania michezo yetu.
Nitakuwa nikiungalia mchezo wa Everton na Man City'

Liverpool watakuwa wakiingia katika mchezo huo huku wakiwa na majeraha ya kipigo cha mchezo wao uliopita ambao walichapwa mabao 2-0 na Chelsea matokeo ambayo sasa yanategemea kikosi cha Manuel Pellegrini kipotezea angalau alama katika michezo yao mitatu iliyosalia ili Liverpool iweze kutwaa taji wakicheza bila kupoteza mchezo.

Rodgers alionekana mwenye hasira kutokana na mbinu za kiuchezaji za Jose Mourinho za kupaki basi licha ya kwamba sasa anamtaka mreno huyo amtakie mema katika michezo ya wikiendi hii.

No comments:

Post a Comment