Big Phil Luiz Felipe Scolari ndio basi tena |
Matarajio ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Luiz
Felipe Scolari, ya kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo
yamaenza kuingia shakani, baada ya viongozi watakao liongoza shirikisho soka
CBF kuanzia mwaka 2015 kuthibitisha hawatokuwa na mpango nae.
Viongozi watarajiwa na chama cha soka nchini Brazil,
wametangaza mpango huo kufuatia Scolari kushindwa kutangaza kujiuzulu kutokana
na kadhia ya kupachikwa mabao saba kwa moja, iliyomkuta siku mbili zilizopita
huko Bero Horizonte mbele ya timu ya taifa ya Ujerumani.
Makamu wa rais wa chama cha soka nchini Brazil, Delfim
Peixoto ambaye atashika hatamu ya uongozi wake kuanzia mwezi April mwaka 2015,
amesema haoni sababu ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 65, kuendelea kuwepo
madarakani kutokana na tabia yake ya kufanya maamuzi binafsi pasina kusikiliza
ushauri wa mtu mwingine.
Peixoto, amekiambia kituo cha televishani cha ESPN Brazil,
kwamba Scolari alikuwa na kila sababu ya kuikwepa aibu iliyowakuta ya
kuchabangwa mabao saba kwa moja, lakini mapungufu yake ndiyo chanzo cha hayo
yote, hivyo anaona muda wa kustahafu kwa kocha huyo umewadia.
Wakati huo huo Luis Philipe Scolari amebadili kauli yake ya
kutotarajia kujiuzulu na kusema huenda akatangaza mustakabali wa nafasi yake
ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Brazil mara baada ya fainali za kombe la
dunia.
No comments:
Post a Comment