Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza mabadiliko ya
kuanza kwa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014-15 ambayo ilikuwa
imepangwa kuanza kutimua Augusta 24 mwaka huu.
Taarifa iliyotumwa katika dawati la mtandao wa Rockersports na afisa habari
na mawasilino wa shirikisho hilo Bonface Wambura inaeleza kwamba mshike mshike wa ligi kuu ya
soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014-15, sasa utaanza kutimua vumbi lake Septemba
20 mwaka huu.
Sababu kubwa iliyoelezwa na TFF ya kusogeza mbele kuanza
kwa ligi ya msimu ujao ni kutaka kupitisha michuano ya klabu bingwa Afrika
Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Michuano ya Kombe la Kagame inayoshirikisha mabingwa wa
nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
itafanyika Agosti mwaka huu nchini Rwanda.
Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu. Timu hizo ni
mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya
City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting,
Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.
Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano
hiyo kuanza kutimua vumbi.
No comments:
Post a Comment