Marcio Maximo kocha wa Yanga ajiwekea utaratibu wa kuongea na waandishi wa habari |
Kocha mkuu wa timu ya Young Africans SC Mbrazil Marcio Maximo amesema
atakua akiongea na waandishi wa habari kila siku ya Ijumaa asubuhi mara
tu baada ya mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ili kuwapa nafasi
na fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maandalizi ya
kikosi chake msimu ujao.
Akiongea na mtandao rasmi wa klabu ya Young Africans Maximo amesema,
ameamua kufanya hivyo ili kupunguza kuwepo taarifa tofauti kuhusiana na
benchi la ufundi pamoja na wachezaji wake katika maandalizi ya msimu
ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.
"Unajua utendaji wa kazi umebadilika, nafasi yangu kwenye klabu na
nilipokua timu ya Taifa ni tofauti, hivyo nimekubaliana na uongozi na
umeniruhusu kuwa naongea na vyombo vya habari kwa pamoja kila siku ya
Ijumaa mara tu baada ya mazoezi ya asubuhi "alisema Maximo
Maximo ameanza kazi ya kukinoa kikosi cha Young Africans tangu mwishoni
mwa wiki iliyopita na kuwatuvia wapenzi, washabik na wanachama ambao
wamekua wakijitokeza kwa wingi kushuhudia ufundishaji wa kocha huyo
mwenye mvuto mkubwa kwenye soka la Tanzania.
No comments:
Post a Comment