Je van Persie atacheza dhidi ya Argentina ? |
Kocha wa Uholanzi Lous van Gaal amezua taharuki baada
ya kusema kuwa mashambulizi wake matata van Persie anaugua utumbo na
kuwa anahofu iwapo atacheza dhidi ya Argentika katika mechi ya pili ya
nudu fainali au la.
Kocha Van Gaal amesema kuwa nafasi yake huenda
ikachukuliwa na Nigel de Jong iwapo daktari wa timu hiyo atadhibitisha
kuwa van Persie huenda akashindwa kuhimili uchungu na hivyo kukosa mechi
hiyo muhimu.
Iwapo de Jong atacheza basi itakuwa mara yake ya kwanza tangu aondoke
uwanjani katika mechi ambayo Uholanzi iliilaza Mexico mabao 2-1 katika
raundi ya kwanza.
Robie Van Persie mashakani usiku wa leo |
Kocha huyo anakila sababu ya kuwa na wasiwasi
baada ya Nahodha wake kutoshiriki mazoezi siku ya kuamkia mechi hiyo
muhimu , hata hivyo anaafueni baada ya kurejea kwa Ron Vlaar na Leroy
Fer mazoezini.
wawili hao walikuwa wamejeruhiwa katika mechi za makundi.
Tegemeo la Argentina Lionel Messi |
Kwa upande wao Argentina wnaendelea na mazoezi yao kikamilifu
ijapokuwa inatarajiwa kuwa Mshambulizi wa Bracelona Lionell Messi
atakabidhiwa majukumu mahsusi ya kuifikisha Argentina katika fainali yao
ya kwanza tangu mwaka wa 1990.
Angel Di Maria |
Argentina pia wanatatizika kwa kumkosa mchezaji
wa kutegemewa Angel Di Maria ambaye amejeruhi paja lake lakini
watakuwa na wasaidizi wake Sergio Aguero na Marcos Rojo ambao watakuwa
kwa ajili ya mechi hiyo ya kihistoria kwao.
Uholanzi tofauti na Argentina imefuzu kwa
fainali ya kombe la dunia mara mbili zilizopita ikimaliza ya pili mara
mbili mfululizo
No comments:
Post a Comment