Douglas Costa (kulia) nafukuziwa na Manchester United na Arsenal |
Arsenal na Manchester United wameambiwa waziwazi kuwa wanapaswa kupandisha dau mpaka kufikia pauni milioni £40 endapo kweli wanataka kumsajili Douglas Costa kutoka Shakhtar Donetsk.
Costa mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na kuondoka Shakhtar wiki zijazo kufuatia kugomea kurejea Ukraine kwasababu ya matatizo ya kisiasa.
Uwezo wake aliouonyesha katika klabu ya Shakhtar umepelekea vilabu vingi barani Ulaya vikiwemo Arsenal na AC Milan ambavyo vimekuwa vikipimana ubavu kudaka saini ya Mbrazil huyo.
Taarifa kupitia gazeti la Daily Stars zimearifu kuwa mashetani wekundu watapaswa kuongeza dau lao mpaka kufikia pauni milioni £40 ili aweze kutua Emirate Stadium msimu huu wa kiangazi huku mabosi wa klabu yake wakisema mshambuliaji huyo ni bora zaidi ya mwenzake Hulk.
Mchezaji mwenyewe anataka zaidi kuelekea Arsenal kuliko kujiunga na United.
No comments:
Post a Comment