Nyota anayewindwa na
Manchester United Juan Cuadrado ataendelea kusalia Fiorentina msimu
huu wa uhamisho wa kiangazi hii ikiwa ni kwa mujibu wa meneja Vincenzo
Montella.
Nyota huyo wa
kimataifa wa Colombia amekuwa akihusishwa na kuelekea United na
Barcelona, baada ya kuonyesha soka safi wakati wa fainali za kombe la
dunia nchini Brazil.
Matumaini ya Man
United kumkamata kiungo huyo yalionekana kupanda zaidi wiki iliyopita
wakati Barca walipojiondoa katika harakati hizo na sasa inavyoonekana
ni kuwa ataendelea kusalia nchini Italia.
‘Sikuwahi kufikiri
kumpoteza Juan. Alikuwepo hapa hapo nyuma na sasa bado yupo na
ataendelea kusalia hapa hapo baadaye’amesema Montella.
‘siadhani kama
stori za Cuadrado zitakwisha.
‘Mchezaji wa aina
yake anaweza kucheza katika kila eneo la kiungo.’
Wakati hayo yakiwa
hivyo , Louis van Gaal bado naonekana kukaribia kusainisha Angel Di
Maria,baada ya bosi wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuonekana kuwa na
mashaka na hatma ya baadaye ya winga huyo.
No comments:
Post a Comment