Inavyoonekana ni kwamba Liverpool inashindwa kupambanua mambo ya kimsingi ya kimakubaliano tangu kuondoka kwa Luis Suarez kwani mpaka hivi sasa ni kwamba uwanja wa Anfield bado unaendelea kumuonyesha mshambuliaji huyo raia wa Uruguay katika bango kubwa lililoko lango kuu la kuingilia uwanjani hapo(Kop stand.

Mshabiki wanasema Suarez ataendelea kuonekana Anfield kama vile ishara ya kuendeleza uwepo wake akiitangaza jezi mpya kupitia bango hilo.
Jumapili ijao Liverpool itakuwa ikifungua msimu dhidi ya Southampton, sasa mashabiki wanasema ifanyike haraka kuondoa tangazo hilo kabla ya mchezo wa Jumapili.
No comments:
Post a Comment