Arsene Wenger anaripotiwa kufuatilia mwenendo wa nyota wa Marseille Florian Thauvin mwenye umri wa miaka 2 kabla ya kufika kwa dirisha la usajili la mwezi Januria.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia gaeti la Star meneja wa Arsenal ameendelea kuweka jicho lake karibu kwa kiungo mshambuliaji huyo kufuatia kiwango chake cha kuvutia cha hivi karibuni akiwa na kigogo hicho cha soka cha nchini Ufaransa tangu kujiunga nayo msimu uliopita.
Wenger amekuwa shabiki wa Thauvin kwa wakati fulani kiasi kupelekea kusema kuwa kiungo huyo ni tegemeo kubwa la Ufaransa katika siku za baadaye.
No comments:
Post a Comment