Mshambuliaji wa Sheffield Ched Evans atoka jela |
Evans (kulia) akiwa katia picha na familia yake |
Nyota wa kimataifa wa Wales ambaye alikuwa akiichezea Sheffield United, ametumikia jela kwa miaka miwili na nusu kufuatia kubaka msichana mwenye umri wa miaka 19 |
Nyota Evans akikutana na mpenzi wake Natasha Massey |
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye aliwahi kuichezea Manchester City alihukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hati ya kumbaka mwanamke kwenye umri wa miaka 19 katika chumba cha hoteli.
Evans, ambaye aliondoka katika jela ya Wymott Prison karibu na Leyland kaskazini magharibi ya nchi ya England mapema hii leo ameahidi kuwa mtu mwema uraiani kuanzia hivi sasa.
Meneja wa Sheffield United Nigel Clough amekuwa akifikiria kama kuna uwezekano wa kumrejesha kundini lakini akikabiliwa na upinzani kutoka kwa watu zaidi ya 145,000
waliosaini kitabu maalumu kupinga kurejea klabu hapo kwa Blades.
Hapo jana naibu waziri mkuu wa Uingereza na mbunge wa Sheffield Nick Clegg
waliitaka klabu hiyo kufikiria kwa makini kabla ya kuamua kumruhusu Evans kuichezea tena klabu yao.
No comments:
Post a Comment