Mabingwa Ulaya Real Madrid watakuwa bila Gareth Bale na Sergio Ramos
kwa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Liverpool Jumatano ya leo kwani
wote wawili waliachwa nje ya kikosi cha Carlo Ancelotti kutokana na
mejaraha.
Bale huenda pia asicheze El Clasico ya kwanza ya msimu huu Jumamosi dhidi ya Barcelona kutokana na jeraha la misuli ya tumboni.
Ramos amekosa mechi tatu za majuzi za klabu hiyo na taifa kutokana na
jeraha la misuli ya sehemu ya chini ya mguu, lakini kutokuwepo kwake
sana ni tahadhari kabla ya safari hiyo ya Barca Bernabeu.
Wachezaji wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema na Raphael Varane,
waliokosa ushindi wa 5-0 Jumamosi Levante kutokana na homa,
wamejumuishwa kwenye kikosi kilichotua Uingereza Jumanne asubuhi.
Madrid wamo kileleni Kundi B baada ya kushinda mechi zao mbili kufikia sasa na wamo alama tatu mbele ya Liverpool na Basel.
No comments:
Post a Comment