ARGENTINA YAISAMBARATISHA JAMHURI YA IRELAND NYUMBANI
Licha ya kucheza wakiwa nyumbani huko Ireland katika dimba la Aviva Stadium timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland imejikuta ikipoteza mchezo mbele ya Argentina .
Wakicheza mchezo huo bila ya kocha wao Giovanni Trapattoni ambaye amefanyiwa upasuaji kikosi hicho kilikuwa kikiongozwa na Robbie Keane akifanya kazi hiyo kwa mara yake ya 100.
Alikuwa ni Di Maria aliyeifungia Argentina bao la pekee katika dakika ya 20 ya mchezo huku Shay Given walinzi wake wakidhani mfungaji alikuwa ameotea.
No comments:
Post a Comment