Hapo anaonekana Zlatan Ibrahimavic akipongezwa ba wenzake Emir Bajrami na Ola Toivonen wa timu ya taifa ya Sweden baada ya kufunga moja ya bao katika ushindi wa mabao 3-0 katika dimba la Rasunda Stadiom huko Sweden
Uwanja wa Wembley ukiwa na watazamaji wachache katika mchezo kati uingereza dhidi ya Hungary ambapo Uingereza ilipata ushindi wa mabao 2-1 huku Uingereza ikicheza kwa mara ya kwanza baada ya kichapo cha aibu toka kwa wajerumani katika fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini hapa inaonekana mashabiki walivyoshindwa kuiunga mkono timu yao chini ya Fabio Capello.
wachezaji wa Wales wakipongezana baada ya kufunga moja ya magoli muhimu katika mchezo wao dhidi ya Luxembourg ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 5-1mchezo ukipigwa katika dimba la Parc y Scarlet huko Wales,Ashley Wiliams namba 6 akifunga bao lake la kwanza na kupongezwa na akina Craig Bellamy
Anaitwa John Taschack katika moja ya matukio ya mchezo wao wa Wales dhidi ya Luxembourg na kuibuka na ushindi murua wa mabao 5-1 wakiutumia mchezo huo pia kujiandaa na mchezo dhidi ya Montenegro kuwania kufuzu fainali za EURO 2012.
Nahodha Steven Gerard akishangilia baada ya kufanikiwa kufunga bao la kuswazisha katika mchezo wao dhidi ya Hungary katika dimba la Wembey na hatimaye mwisho wa dakika 90 Uingereza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Gerald akiendelea kushangilia kwa staili ya kupaa angani
Fabio Capello akipozi katika moja ya tukio kuangalia namna mchezo ulivyokuwa ukiendelea
Huu ni mchezo kati ya Montenegro dhidi ya Ireland ya kaskazini ambapo Montenegro walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 ambapo kocha Nigel Worthngton alikuwa akipima kikosi chake huko Podigorica katika dimba la Pod Poricom
Hawa ni wachezaji wa Luxembourg wakijifariji na bao lao moja dhidi ya Wales na kupoteza mchezo huo.katika rank za fifa hawa wapo katika nafasi ya 117 sasa sijui baada ya matokeo ya kichapo cha jana cha mabao 5-1 watakuwa wamejiweka katika nafasi gani.
Huu bado ni mchezo kati ya Wales dhidi ya luxembourg, kumbuka bao la kwanza lilikuwa la mkwaju wa penalt likifungwa na Joe ledley huku katika picha akionekana kiungo wa Leicester city Andy King akifanikiwa kufunga bao lake la kwanza kimataifa baada ya pasi murua toka kwa Graig Bellamy
No comments:
Post a Comment