KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 12, 2010

Evander Holyfield kuzipiga November

Evander Holyfield anataraji kuzipiga dhidi ya Sherman "The Tank" Williams kunako November 5 ikiwa ni siku chache baada ya bingwa huyo wa zamani wa masumbwi kukamilisha jumla ya miaka 48.

Meneja wake Ken Sanders amekaririwa jumatano hii akisema amepokea karatasi zilizo sainiwa toka kwa Williams mwenye umri wa miaka 37 akitaka pambano hilo la round 12.

Sanders amesema pambano hilo litapigwa katika ukumbi wa Joe Louis Arena huko Detroit.Anasema Holyfield na kampuni ya kibishara inayohusina na maandalizi kama watakutana na maafisa wengine kadhaa kwa ajili ya kukamilisha mpango mzima.

Holyfield ambaye ana rekodi ya 43-10-2, 28 KOs atakuwa anaingia ukumbini baada ya kumchapa kwa knockout katika round ya nane Francois Botha katika pambano lililopigwa April 10 huko Las Vegas huku Holyfield akidai angalau kijitaji.

Lilikuwa ni pambano la kwanza kwa Holyfield tangu kuingia katika malumbano ya kupoteza pambano lake dhidi ya mshika mkanda Nikolai Valuev pambano ambalo lilipigwa Switzerland December 2008.

Licha ya umri wakw kumtupa mkono bado , Holyfield amekuwa akitaka mapambano kadhaa na Sanders anasema ushindi dhidi ya Williams unaweza kutoa nafasi nyingine ya bondia wake Holyfield kumtaka “titleholder” Vitali Klitschko.

No comments:

Post a Comment