KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 11, 2010


MISS WORLD 2010

Inner Mongolia itakuwa ni mwenyeji wa michuano ya kusaka mrembo wa dunia maarufu kama Miss World mwezi October

Licha ya kwamba fainali ya 2010 Miss World itafanyika kule Sanya,hii ni miongoni mwa mambo ni ya kuvutia na kufurahisha kuwapa fursa washiriki wa shindano hilo kuelekea katika safari ya utalii kwa takribani mwezi mzima huko China.baada ya kuwepo katika jiji la Beijing,wawakilishi wa shindano hilo watasafiri kuelekea Inner Mongolia katikamji wa Ordos.
Mwenyekiti wa kama ya maandalizi ya Miss World Julia Morley anakaririwa akisema
“Ordos ni eneo jipya na zuri katika maendeleo mapya ndani ya china ambapo serikali za maeneo huko China zimekuwa zikiimarisha maeneo mbalimbali yenye mvuto wakipanda miti ya kuvutia katika maeneo mbalimbali kuleta mvuto.

Miss World 2010 inarejea Sanya nah ii itakuwa ni mara ya tano katika fainali hizi ambazo zitakuwa ni za 60 na kufanyika huko katika jimbo la Hainan

Mwaka mashindano hayo ya mwaka huu yatafanyika jumamosi ya ya Octoba 30 katika mji wa Sanya uliopo katika jimbo la Hainan.

Washiriki kutoka katika mataifa 120 watakuwa wakishiriki wataanza na kile kinachotambuliaka kama Miss World’s diamond anniversary year.wiki nne za kwanza wakizuru China katika maeneo ya kuvutia huku wakisubiri siku ambayo ni maalum ambapo dunia nzima itakuwa ikishuhudia kupitia luninga katika “tropical paradise”, Sanya.

Shindano la kusaka mrembo wa dunia limekuwa likipata umaarufu duniani tangu kuzinduliwa kwake mwaka 1951 na limekuwa ni tukio la mwisho wa mwaka likipata watazamaji takribani bilioni moja duniani kote. Katika shindano hili warembo hushindana katika nyanja mbalimbali ikiwemo urembo , fashion,vipaji na utamaduni.

Kwasasa hapa nyumbani tanzania ndiyo kwanza maandalidi yameenza katika kumsaka mwakilishi wa tanzania katika kumsaka mrembo wa dunia huku mswali mengi yakiwa ni nani atakuwa mwenye bahati ya kuiwalisha nchi na nini atavuna huko China.

Pengine hili limekuwa swali ni nini sababu ya Tanzania kutokufanya vizuri miaka nenda miaka rudi katika kinyang'anyiro hiki cha dunia.

licha ya zawadi kuwa ni za kuvutia na changamoto nyingine toka kwa wadhamini wa shindano hili kwa hapa nyumbani Tanzania bado kilio cha mafanikio ya urembo hakina mnyamazishaji .Kwasasa nchi mbalimbali duniani zimeshakamilisha zoezi la kumpata mwakilishi wao kwa hapa barani Afrika ni pamoja na Nigeria, Ivory coast, Namibia , Zimbabwe ,Afrika kusini,Zimbabwe na Zambia lakini Tanzania ndiyo kwanza warembo wameanza kambi ya kutafuta mrembo wa taifa huku mashindano ya dunia yakitarajiwa kufanyia ocktoba 30 kule Sanya sasa sina hakika kama kuna muda wa maandalizi ya mrembo kabla ya kuelekea huko Sanya wakati bado kuna muda wa kutembelea vivutio mbalimbali huko China kuanzia mwanzoni mwa mwezi ocktoba.



No comments:

Post a Comment