THEO WALCOTT AKIMBIZWA HOSPITALI NA KUMPA WASIWASI ARSENE WENGERWinga wa Arsenal Theo Walcott amelazimika kukimbizwa hospitali kufuatia kupatwa na maumivu yaliyotokana na mchezo kati ya uingereza dhidi ya Switzerland usiku wa huamkia hii leo
Mshambuliaji huyo wa Arsenal Theo Walcott amepelekwa hospitali kufuati maumivu ya ankle na hivyo kutakiwa kufanyiwa vipimo vya x-ray kuangalia ni maumivu kiasi gani atakuwa amepata.
Walcott amepata maumivu hayo katika guu lake la kulia katika harakati za kujaribu kutengeneza goli la ufunguzi la Wayne Rooney katika dakika ya 10 ya mchezo . Walcott alianzisha move ya goli baada ya kupeleka pasi murua kwa Glen Johnson toka upande wa kulia kabla ya mlinzi huyo wa kulia wa Liverpool Johnson kusukuma pasi kuelekea katikati kwa Rooney na Roony kuukwamisha mpira wavuni likiwa na bao lake la kwanza ndani ya michezo 12 ya kimataifa.
Walcott amekuwa katika majeruhi kwa muda sasa katika kikosi cha washika bunduki Asernal na huenda hili likawa ni pigo jingine kwa Arsene Wenger baada ya taarifa kuwa mshambuliaji wake mwingine Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita.
Katika mchezo wa jana alibadilishwa na mshambuliaji wa pemben I wa Manchester City Adam Johnson.
Jermaine Defoe pia alikumbwa na maumivu kama hayo alipokuwa akijaribu kutengeneza bao la pili lililowekwa kimiani na Adam Johnson. Mshambuliaji huyo wa Spurs naye alibadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Darren Bent lakini hajawa wazi ni maumivu kiasi gani Defoe amepata licha ya kwamba amekuwa majeruhi wa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment