KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 13, 2010

LIVERPOOL YAJIKOMBOA TOKA KATIKA MINYORORO YA WAMILIKI WA KIMAREKANI

Liverpool yaongoka
Tom Hicks na George Gillett wameshindwa katika kesi iliyokuwa katika mahakama kuu ya London katika jaribio lao la kutaka kuendelea kusalia madarakanani kuingoza Liverpool.
Wamerekani hao ambao hawana umaarufu mkubwa huko Marekani walikuwa katika jaribio la kuwaondosha baadhi ya watu waliokuwa katika bodi ya klabu waliokuwa wapinzani wakubwa katika ndani ya bodi wakipinga kuuzwa kwa Liverpool kwenda kwa New England Sports Ventures (NESV).
Lakini Mr Justice Floyd amenyoosha hali ya mambo na kusema jamaa hao hawakuwa na nguvu ya kufanya hivyo.
Maamuzi hayo yana maana kuwa mchakato wa taratibu za mauuzo ya klabu kwenda kwa mmiliki mpya NESV yanaweza kuendelea licha ya mwenyekiti wa klabu hiyo Martin Broughton akiweka wazi kuwa bids ama offer nyingine pia zinaweza kujadiliwa katika kikao cha hii leo.

Akikaririwa wakati anatoka katika mahakama ya Royal Courts iliyoko London hii leo Broughton anasema
"bila shaka ni wazi kuwa leo ni siku muhimu sana kwa klabu yetu,"
"hatua hii itaweka wazi njia ya kuelekea kuuzwa kwa klabu na tutakuwa na kikao cha bodi jioni ya leo kujadili kuelekea kwenye mchakato.
Maamuzi ya Mr Justice Floyd yamekuwa ni yanaonyesha wazi kuwa Broughton na wawekezaji wa Royal Bank of Scotland watakuwa katika matumaini makubwa sasa
"kilikuwa ni kipindi kigumu lakini sasa tumekuwa confident. kama unavyojua ukienda mahakamani huwezi kuwa na uhakika."
Kuelekea kuuzwa NESV Broughton ameongeza kwa kusema
"bodi italazimika kutazama tena katiba lakini siwezi kusema au kutoa maamuzi yoyote juu ya bodi itasema nini. Si sawa kutoa maamuzi ya kile ambacho bodi inafikiria kusema .
"lakini ni kwamba klabu inaelekea katika wakati mzuri, tutarekebisha na kuimarisha misingi ya haki ndani ya klabu.
"deni kubwa ambalo limekuwa likituzonga sasa litaondoshwa na tunakwenda katika kipindi kizuri kwani tutakuwa na wamiliki wa ukweli kwa mashabiki."
John W Henry,ambaye ni kiongozi wa NESV kwa upande wake amefurahia maamuzi ya High Court kupitia mtandao wake wa Twitter na kumpongeza mwenyekiti wa klabu Broughton,mkurugenzi Christian Purslow mkurugenzi wa biashara Ian Ayre.
Akikaririwa anasema
"Well done Martin, Christian & Ian. Well done RBS. Well done supporters!"
NESV sasa inaelekea kukamilisha kutoa malipo ya offer yao ya pauni milioni 300 ambayo inatosha kulipa madeni ya pauni milioni 240 klabu hiyo ilikuwa ikidaiwa na kiasi cha pauni milioni 40 ada walikopa toka Royal Bank of Scotland. Kimsingi offer yao imekubaliwa na klabu.

Lakini wakati hayo yakiwa hivyo tayari offer nyingine imearifiwa kutolewa hapo jana (materialized) toka kwa bilionea toka pande za Singapore Peter Lim ya pauni za kingereza milioni 320 taslimu kukamata klabu hiyo na pia akitenga nyingine pauni milioni 40 kwa lengo la kununulia wachezaji ,mungu awape nini “gunia la chawa”

No comments:

Post a Comment