KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, October 12, 2010

MOURINHO APUUZIA UKOSOAJI WA MASHABIKI WA REAL MADRID Mourinho katika ukosoaji mkubwa madrid
Jose Mourinho amesisitiza hana matatizo na ukosoaji akiwa Real Madrid lakini ametanabaisha kuwa bado anapendelea kufanya kazi hapo
Mourinho akemuwa katika mazingira magumu ndani ya Madrid licha ya ushndi toka kwa Espanyol na Deportivo lakini safu ya umeonekana imeonekana katika wakayti mgumu kupata mabao.
Kama kocha mwenye kucheza soka la kujilinda zaidi Mourinho ameonekana sasa kuwa na matatizo katika kupata mabao kiasi kukumbana na ukosoaji wa mashabiki wa klabu hiyo lakini mwenyewe akipuuzia.

MAAMUZI YA KUUZWA KWA LIVERPOOL NI JUMATANO HII

Mashabiki wa Liverpool wanaendelea kusubiri maamuzi mazito ya kuuzwa au kutokuuzwa kwa klabu yao jumatano asubuhi maamuzi ambayo yatakuwa ni hatma ya baadaye ya klabu hiyo .
Hata hivyo hakuna guarantee yoyote kama hakimu atakuwa amelalia upande upi katika ya pande mbili zinazo pingana.
Mahakama kuu ya London imekuwa katika hali tete kiasi kuvuta hisia za mashabiki jumanne ikisubiriwa kutoa maamuzi wakati boardroom ya Liverpool ikiwa katika mvutano wa pande tatu Hicks na Gillett,bodi ya klabu yenyewe na Royal bank ya Scotland.
Richard Snowden QC mtendaji wa RBS anawashutumu wamiliki pacha wa Marekani kwa kile kinachoitwa "breathtaking arrogance" yaani madharau na kusababisha mkanganyiko wa sheria za mauzo kwa kujaribu kumuondosha mkurugenzi wa mambo ya kibiashara Ian Ayre na mkurugenzi mtendaji Christian Purslow toka katika bodi juma lililopita
Hicks na Gillett wanapinga kwa klabu hiyo kuuzwa kwa endapo mauzo hayo yatafanyika basi wazi wao watapoteza karibu pauni milioni 144 .
Ayre na Purslow wanaungana na mwenyekiti wa klabu hiyo Martin Broughton kupiga kura ya kuunga mkono kuuzwa kwa klabu kwa New England Sports Ventures, na kama mahakama itaridhishwa na bank kuona sawa basi ni wazi mipango mingine ya makabidhiano itakuwa huru kuendelea .


Serikali ya Tanzania yataka nyimbo za taifa sasa zipigwe kwa brass band baada ya kumbwela katika mchezo wa timu ya taifa ya tanzania dhidi ya Morroco
Serikali imelitaka Shirikisho la soka nchini TFF kupiga nyimbo za taifa katika michezo yote ya kimataifa kwa kutumia “brass band” badala ya CD kama ilivyokuwa imezoeleka.

Tamko hilo la serikali limekuja kufuatia kutopigwa kwa nyimbo za taifa kabla ya kuanza kwa mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali ya mataifa ya Afrika kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Morocco uliofanyika jumamosi katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na badala yake nyimbo hizo zikapigwa mara baada ya timu hizo kutoka mapumziko kinyume na utaratibu.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Seth Kamuhanda amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo ambalo limetokea mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ni la aibu kwa Nchi nzima kwa ujumla.

Tamko la Serikali linafuatia maamuzi mazito ya Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kupitia kwa Rais wake Leodger Tenga kutangaza kumsimamisha Afisa habari wake FLORIAN KAIJAGE kutokana na tukio hilo wakati uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.

Tamko la serikali la kupigwa kwa brass band limetolewa katibu kuu wizara ya habari utamaduni na michezo Sert Kamhanda kwa niaba ya Waziri wa Habari utamaduni na Michezo George Huruma Mkuchika
Katika hatua nyingine Kamuhanda amesema mitambo ya kuchezesha CD katika uwanja huo wa taifa ni mizuri na wala haina tatizo lolote na wameshangazwa na kauli ya TFF kuwa kulikuwa na matatizo katika mitambo hiyo.

No comments:

Post a Comment