KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 6, 2010




Bosi wa Chelsea Carlo Ancelotti amewaza na kuwazua na sasa ameanza kupatwa na wasiwasi na kiwango cha timu yake hususani katika kipindi cha mchezo wa jana dhidi ya Everton mchezo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Katika jumla ya michezo sita iliyopita ya ligi kuu ya kandanda nchini uingereza “The Blues” Chelsea imefanikiwa kupata points tano na kushindwa kuchomoza na ushindi katika michezo mine iliyopita.
Akikaririwa anasema
"tulianza kuwa na wasiwasi baada ya mchezo kuanza kufuatia wapinzani wetu Everton kuanza mchezo kwa pressure kubwa
Mabingwa watetezi walianza kwa makeke ligi hiyo kwa ushindi wa michezo mitano mfululizo na ndani ya michezo hiyo mitano walifanikiwa kupata idadi kubwa ya mabao yapatayo 21 lakini hali ya mambo kwasasa imekwenda mrama baada ya kutereza na sasa wakijikuta katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi .

Katika mchezo wa jana alikuwa ni Didier Drogba aliyewaweka Chelsea katika uongozi wa mchezo kwa njia ya mkwaju wa penalty kabla ya Everton kupitia kwa Jermaine Beckford aliyetokea benchi kusawazisha kwa kichwa dakika nne kabla ya muda wa kawaida wa mchezo kumalizika.
Anasema Ancelotti
"kipindi cha pili kilikuwa kibaya hatukucheza kama tulivyokuwa tunatarajia zaidi ya kucheza mipira mirefu ambayo hatukuwa tumejipanga kucheza hivyo.

Bosi wa Arsenal Arsene Wenger ampongeza Samir Nasri


Bosi wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa Samir Nasri atakuwa katika kiwango bora baada ya kufanikisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham ushindi ambao umeiweka Arsenal katika kilele cha msimamo wa ligi kuu ya kandanda nchini uingereza “Premier League”.
Arsenal imejiweka katika uongozi wa ligi hiyo baada ya matokeo mengine ya ligi hiyo yanayo vihusu vigogo vya ligi hiyo Chelsea na Manchester United kwenda ndivyo sivyo, Wao Chelsea wakienda sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton na mchezo wa Manchester United dhidi ya Blackpool kuahirishwa kufuatia kushuka kwa theluji kwa wingi
Akikaririwa bosi wa Arsenal Wenger anasema
"kinachotakiwa kwasasa mimi kama meneja ni kupata yaliyo mazuri kutoka kwa wachezaji wangu,"
"kuhusu Samir Nsri kuna mengi natarajia kutoka kwake, wengi wanauliza kuhusu yeye lakini kiukweli ni kwamba anakipaji cha kipekee."

Bosi wa Man City Roberto Mancini alalama juu ya umaliziaji mbovu wa kikosi chake


Bosi wa Manchester City Roberto Mancini ametaka kikosi chake kufanya kazi ya ziada kuimarisha uwezo wa kumalizia mipira ya mwisho na kuweka nyavuni gozi la ngom’be baada ya kushuhudia vijana wake wakimbwela katika kumalizia mipira ya mwisho na kuonyesha ubutu wa kumaliza katika mchezo wa jana dhidi ya Bolton.
City ilipoteza nafasi nyingi za kumalizia baada ya kupata bao la kuongoza kupitia kwa Carlos Tevez bao lilisalia mpaka dakika tisini za mchezo zinamalizika.
Akikaririwa Mancini anasema
"wakati mwingine tulikuwa wabinafsi mno tulikuwa tuna piga mashuti sehemu ambayo tulipaswa kutoa pasi lazima kubadilishe hali ya mambo
"tunapo kuwa na nafasi lazime tufunge kama mimi ningekuwa nacheza basi ningekuwa na nafasi ya kupata angalau mabao mawili ama matatu."

Matokeo hayo ya City ya hapo jana ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bolton yanaiweka katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza Premier League.

Kuhusiana na kura za fifa za kombe la dunia afisa wa FA ya uingereza Alex Horne ataka mabadiliko ya mfumo wa kura
Baada ya zoezi la kura za maamuzi kuelekea katika maandalizi ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 na 2022 kuwa limemalizika bado waingereza wanaonekana kuumia zaidi baada ya fifa kutoa ridhaa kwa mataifa ya urusi na Qatar kupenya na kupewa ridha ya maandalizi.
Waingereza wanataka matumizi na hatua ya awali ya mchujo kubadilika .
Alex Horne mtendaji mkuu wa FA ya uingereza amekaririwa akisema
"nadhani mchakato unatakiwa kufanyiwa mabadiliko,"alikuwa akizungumza na BBC Radio 5 live.
Anaendelea kwa kusema
"kwa mfano wako washindani tisa sasa washindani hawa wote tisa kwenda Zurich kuna ulazima gani"

Horne amekuwa katika nafasi ya utendaji tangu mwezi May baada ya kushikilia nafasi hiyo kama kaimu , anasema kulikuwa hakuna haja ya washindani wengi kuelekea Zurich kama kamati ya ufundi ilisha toa maelezo ya awali katika ripoti yao ya ufuatiliaji.













Cesc Fabregas kurejea dimbani katika mchezo dhidi ya United
Nyota wa Arsenal skipper Cesc Fabregas ana matarijio ya kurejea dimbani katika mchezo wa ligi ya uingereza dhidi ya mashetani wekundu mchezo ambao unatarajiwa kufanyika jumatatu ya wiki ijayo baada ya jumatatu ya kesho.
Timu hizo mbili zilizo katika nafasi ya juu ya msimamo wa ligi zinatarajia kukutana Old Trafford jumatatu ya December 13.
Mchezo huo unatazamwa kama ni mchezo ambao kwasasa vijana wa Arsene Wenger wakiwa katika ubora ukilinganisha na vijana wa sir Alex Furguson huku “the Gunners” wakiwa na njaa ya kutwaa taji hili kwa mara ya kwanza tangu kipindi kirefu kupita.
Matumaini ya nahodha Fabregas kurejea dimbani yanaonekana kuwa ni makubwa baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na matatizo ya msuli aliyo yapata katika michuano ya UEFA mchezo dhidi ya Braga wiki mbili zilizo pita huku marejeo yake yakionekana kama ahueni kwa Gunners.

Jose Mourinho anaamini kuwa tahadhari ilikuwa muhimu katika mchezo wao dhidi ya Valencia

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho ametetea uwamuzi wake wa kucheza mchezo wa jana wa mfululizo wa ligi kuu ya kandanda nchini Hispania dhidi Valencia kwa tahadhari kubwa na hatimaye kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 .
Mbinu ya Mreno huyo katika mchezo mchezo wa jana ya kucheza kwa tahadhari ilipelekea wachezaji wake kucheza mchezo kwa kutokujiamini baada ya kichapo cha mabao 5-0 kule Camp Nou jumatatu iliyopita .
Akikaririwa Mourinho anasema
"kilichokuwa muhimu kwetu katika mchezo huo ni ushindi kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu na kulikuwa hakuna kingine cha ziada zaidi ya ushindi hasa baada ya kupoteza vibaya jumatatu."
"tulikuwa hatuna kujiamini tena kwa hiyo muhimu ni kuondoa hali ya wasiwasi ili kuondoa dhahma nyingine kwa hiyo niliibadilisha timu .”

Mourinho hapo jana alikwenda kuwapongeza Alvaro Arbeloa na Raul Albiol ambao waliingia kuchukua nafasi za Ricardo Carvalho na Sergio Ramos huku akikaririwa akisema .
"kiukweli si kwasababu ya Ramos na Carvalho walikuwa wanahusika na hali mambo hapo kabla isipokuwa ni kwasababu nilikuwa naona nina Arbeloa na Albiol ambao ni watu serious na wanaojituma . Albiol alikuwa fantastic. Hakukuwa na tatizo kwa Ramos na Carvalho lakini ni kwasababu walioingia walikuwa wanakwenda kufanya yale ya msingi."

No comments:

Post a Comment