KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 6, 2010

FUS Rabat yaichapa Sfaixen na kutwaa taji la michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika

FUS Rabat inakuwa ni timu ya pili toka morocco kutwaa taji la michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kufanikiwa kuichapa kwa mabao 3-2 CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa pili wa marudiano .
Wa-Tunisia ndio waliokuwa na nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo baada ya kifanikiwa kupata sare ya bila mabao katika mchezo wa kwanza uliofanyika Rabat lakini kufuatia matokeo hayo sasa wameangukia pua.
Abdelfatteh Boukhriss ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipa uonguozi FUS katika dakika za mwanzoni mwa mchezo.
Hamdi Rouid alifanikiwa kusawazisha kabla ya Kamel Zaiem kuipatia timu yake bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penalty kipindi cha pili na kuwarejesha wenyeji katika control ya mchezo.
Hata hivyo Mohamed Zouidi alifanikiwa kusawazisha katika dakika ya 74 na kupiga linguine katika dakika ya 89 na kuwa ndio bao la ushindi kwa timu yake katika mchezo ambao umehudhuriwa na watazamaji takribani 30,000.

Katika hatua ya makundi timu hizo zilikutana ambapo Sfaxien ilifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 3-0.
Kumbuka katika michuano ya vilabu bingwa watunisia wengine wa Esperance walikubali kichapo cha mabao 6-1 ukiwa ni ushindi wa jumla toka kwa TP Mazembe ya Congo kiasi sasa kuwafanya watunisia kujiona si wenye bahati katika mwaka huu unaomalizika ukiwa umesaliwa na siku 26.
Kwa matokeo hayo TP Mazembe watakutana dhidi ya wamorocco wa FUS Rabbat katika mchezo wa African Super Cup mchezo ambao utapigwa mwezi ujao yaani January.

No comments:

Post a Comment