KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 6, 2010

Hispania wanasema: Andres Iniesta, Lionel Messi na Xavi ni wachezaji watatu bora katika mwaka wa 2010 lakini swali ni je wanastahili tuzo ya FIFA ya Ballon d’Or?

Imeelezwa na kutangazwa kuwa nyota watatu wa Barcelona Andres Iniesta, Lionel Messi na Xavi wametajwa kuwania tuzo ya FIFA ya Ballon d’Or,kama ilivyotanabaishwa na jopo la makocha wa timu za taifa na waandishi wa habari .
Ingawa huu ni mwaka wa kwanza kwa tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa dunia kuchomoza kwa muunganiko na tuzo iliyokuwa maarufu duniani iliyoasisiwa nchini Ufaransa ya Ballon d’Or, hii inakuwa ni mara ya tatu kwa wachezaji watatu wa timu moja kumaliza kama wachezaji watatu baada ya kikosi cha Milan katika miaka ya mwishoni ya 80 kutawala tuzo hizo hususani katika miaka ya 1988 na 1989 katika tuzo za Ballon d’Or.
Lakini kama ilivyo kawaida kutaibuka mijadala mikubwa kutabiri ni nani ataibuka mshindi wa tuzo hiyo.
Wengi wanaamini kiungo mchezeshaji wa timu ya taifa ya uholanzi Wesley Sneijder ataibuka mshindi miongoni mwa watatu hao na kuibuka na ushindi wa tuzo.
Diego Forlan toka klabu ya Atletico Madrid ambaye ni shijaa wa klabu hiyo katika kuipeleka klabu yake katika mafanikio ya michuano ya Europa League msimu uliopita kama alivyo fanya hivyo katika michuano ya kombe la dunia nchini Afrika kusini akiwa na timu ya taifa ya Uruguay na kuipa nafasi ya nne naye anapewa nafasi kubwa katika kutwaa tu zo hiyo.
Wako pia walinda milango kama Iker Casillas na Julio Cesar walifanya miujiza katika hatua ya vilabu na mataifa ndani ya mwaka 2010. Lakini hata hivyo inaonekana wanne kati hao katika orodha ya mwisho ya wachezaji 23 wanaoekana kuwa na nafasi kubwa kama ilivyo kwa akina Iniesta, Messi na Xavi

Lakini wakati hayo yakiwa hivyo Rais wa Inter Milan Massimo Moratti anasema Lionel Messi, Andres Iniesta na Xavi hawastahili tuzo hiyo na kwamba anayestahili tuzo hiyo ya Ballon D'Or ni Wesley Sneijder
Akizungumza muda mfupia baada ya majina ya wachezaji 23 wa orodha ya mwisho kutangazwa Moratti amesema
"I find it very unjust, Sneijder had a phenomenal season and he won everything he could have, for me he deserved to win the Ballon d'Or.
"I think that is very unjust that the award is given to someone who did not perform the whole year even if we are speaking about a great player."

No comments:

Post a Comment