
Tangazo la kufutwa kazi kwa meneja huyo limekuja baada ya Newcastle kupoteza mchezo wake mbele ya West Brom kwa kichapo cha mabao 3-1 matokeo ambayo yameiweka klabu hiyo katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza “Premier League”.
Hughton ambaye ana umri wa miaka 51 aliingoza Newcastle mpaka kufikia nafasi ya juu msimu uliopita baada ya kuwa katika hali mbaya katika msimu wa 2008-09 .

Taarifa imesema
"bodi ingependa kuweka rekodi na tunatoa shukurani kwa Chris kwa kipindi chote alichokuwepo klabu hapa tangu katika michuano ya Championship mpaka katika Premier League "
No comments:
Post a Comment