
Venue: SAP Arena, Mannheim Date: Saturday 11 December
Mwanamasumbwi toka Uingereza Dereck Chisora amemnyanyapaa kiuwezo Wladimir Klitschko kwa kusema huko nyuma Klitschko alikuwa akikutana na wapinzani ambao wanafanana "taxi drivers" ikiwa ni kuelekea katika pambano lao la jumamosi la kuwania mikanda miwili ya uzito wa juu pambano ambalo linasubiriwa na mamia kwa maelfu ya wapenzi wa mchezo huo duniani jumamosi.
Chisora mwenye umri wa miaka 26 atakuwa akikutana na Klitschko raia wa Ukrain mwenye umri wa miaka 34 na kumpa changamoto ya aina yake bingwa huyo wa mataji mawili ya uzito wa juu ya IBF na WBO .
Pambano hili limepangwa kufanyika nchini Ujerumani katika jiji la Mannheim, Germany.
Akikaririwa chisora motto wa jiji la London anasema
"huu sasa ndio wakati wake wa yeye kupata pambano la kweli ,"
"unaelekea sasa kuanguaka na mimi kuinuka, hukuwahi kupambana na mwanamasumbwi wa aina yangu . I am young, I move my feet, I am fast. I am a different heavyweight."
Katika kujibu kebehi za Chisora , Klitschko amemuelezea Chisora akisema ni bora kuliko mwenzake wa nchi moja ya Uingereza anamzungumzia David Haye akisema hiyo ni kwasababu anaonekana kugeukia vizuri katika masumbwi.
Katika mkutano wao na wana habari jana jumatatu Klitschko anasema "jamaa ni special man akiwa na skills za kutoshad," .
No comments:
Post a Comment