KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 6, 2010

Tuzo za mchezaji bora wa BBC barani African nani kuibuka na tuzo ya mwaka huu?
Gyan, Ayew, Eto'o, Toure na Drogba wametangazwa kuwania tuzo hiyo
Wapenzi wa kandanda duniani bado wana nafasi ya kupiga kura ya kumpendekeza mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2010 zoezi ambalo litakamilika ijumaa ya tarehe 10.
Ndani ya tuzo hizo kuna wachejazi mahiri na tishio watano ambao wanawania tuzo hiyo ambao ni Asamoah Gyan na Andre 'Dede' Ayew, wote wakitokea nchini Ghana .
Toka Cameroon na Inter Milan ni mshambuliaji Samuel Eto'o, ilhali toka katika klabu ya Manchester City kuna kiungo raia wa Ivory coast Yaya Toure sambamba na mwenzake wa taifa moja Didier Drogba,ambaye anakipiga katika klabu ya Chelsea..
Hata hivyo kuelekea katika utoaji wa tuzo hiyo imeelezwa kuwa haitakuwa ni chaguo la moja kwa moja .

Mshindi wa tuzo hiyo anatarajiwa kutangazwa December 17 kupitia BBC's African sports programme.
Mshindi wa mwaka jana wa tuzo hiyo kwa mwaka jana ni Drogba akiipata tuzo hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa wa mabao kwa klabu yake ya Chelsea na timu ya taifa ya nchi yake kwa mwaka jana.
Washindi wa tuzo hiyo katika miaka ya nyuma ni hawa hapa chini

2009 - Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
2008 - Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Egypt)
2007 - Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)
2006 - Michael Essien (Chelsea & Ghana)
2005 - Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)
2004 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2003 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2002 - El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)
2001 - Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
2000 - Patrick Mboma (Parma & Cameroon)

No comments:

Post a Comment