Inter Milan yaichapa TP Mazembe na kutwaa taji la kombe la dunia la vilabu
Ikiwa chini ya kocha Rafael Bernitez, Inter Milan ya Italia imefanikiwa kutwaa taji la kwanza chini ya kocha huyo kwa ushindi ulionerkana kama ushindi mwepesi dhidi ya klabu bingwa barani Afrika toka TP Mazembe baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo ulipigwa huko Abu Dhabi.
Samuel Eto'o alikuwa wa kwanza kutengeza kutengeneza bao la kwanza baada ya pasi murua ilikwenda kwa mfungaji Goran Pandev kabla ya yeye mwenyewe Eto’o kuongeza la pili naye Joseph Biabiany kumalizia bao la tatu .
Mzembe iliyokuwa dimbani bila ya mashabiki wa kuwapa support kama ilivyo kwa wapinzani wao walifikia katika hatua hiyo ya fainali baada ya kuichapa Internacional ya Brazil jana ilishindwa kuonyesha uwezo na kuonekana si timu ya kutisha.
Mshambuliaji hatari wa Mazembe Dioko Kaluyituka licha ya kupata nafasi nyingi na nzuri alishindwa kumalizia mipira ya mwisho .
Mabao ya washindi ya mapema yalikuwa mwiba kwa Mazembe kiasi kumpa nafasi Eto'o kuivunja ngome ya Mazembe na kutengeneza bao la kwanza na Javier Zanetti kulitengeneza bao la pili ambalo lilifungwa na Eto’o.
Muteba Kidiaba aliokoa mipira miwili ya hatari ya Diego Milito na kuwanyima nafasi kigogo cha kandanda nchini Italia.
Kabla ya mapunziko Wakongolese walipata nafasi nzuri pale shuti kali la Kaluyituka lilipo zuiliwa na Ivan Cordoba.
Baada ya mapumziko Maicon wa Inter Milan alishindwa kuweka kimiani gozi la ngombe baada ya kupiga nje ya mlingoti naye Kaluyituka kukosa nafasi nyingine baada ya kulihama lango la wapinzani nakujiweka katika kona ambayo si rahisi kupata bao .
Julio Cesar mlinda mlango wa Inter aliokoa mpira wa “chop” ama “volley” aliyopiga yeye mwenyewe na kuwa ni nafasi ya mpira wa mwisho kwa Mzembe
Ushindi wa ushindi wa Inter unawapa taji lingine baada ya mataji mwengine ikiwa ni pamoja na ligi ya mabingwa , Italian league ,Italian Cup, pamoja na European and Italian Super Cups mataji ambayo wanaendelea kuyashikilia.
TP Mazembe Englebert: Kidiaba, Kaliyutuka (Ndonga 89), Kimwaki, Kasusula, Nkulukuta, Kabangu, Bedi, Mihayo, Ekanga, Kasongo (Kanda 46), Singuluma.
Subs Not Used: Bakula, Tshani, Mwepu, Mabela, Sunzu, Mvete, Kanyimbo, Kayembe, Ngome.
Inter Milan: Julio Cesar, Chivu (Stankovic 54), Maicon, Cordoba, Zanetti, Lucio, Motta (Mariga 87), Cambiasso, Eto'o, Milito (Biabiany 70), Pandev.
Subs Not Used: Castellazzi, Sneijder, Muntari, Materazzi, Alibec, Benedetti, Santon, Nwankwo, Orlandoni.
Barca inapanga kuswap wawili Torres na Fabregas
Barcelona inapanga kutumia ndani ya mamilioni yao ya pauni £85 kuwanasa wawili Cesc Fabregas na Fernando Torres majira ya kiangazi yajayo.
Catalan itakumbukwa ni hivi karibuni tu imefanikisha mkataba wao mnono wa udhamni toka kwa Qatar Foundation mkataba ambao unathamani ya pauni za kingereza milioni £125 ukiwa ni mkataba wa miaka mitano.
Kwa mujibu wataarifa zilizo andikwa katika gazeti la Daily Mirror klabu hiyo imeweza kujiimarisha kiuwezo wa kifedha na sasa ikionyesha matamanio yao ya wakali kadhaa ambao huko nyuma kidogo hali ilikuwa ikiyumba na sasa ndoto zao za kuwanasa na kuwapeleka Nou Camp wazaliwa hao wa Hispania zikionekana kutaka kuwa kweli.
Huko nyuma Fabregas alikuwa anakaribia kujiunga na Barcelona kiangazi iliyopita lakini kukatokezea transfer saga iliyomalizika kwa midfielder kuji-commit tena klabu yake ya Arsenal.
Kwasasa Torres anaonekana kuanza kuchanganywa na maisha ya Anfield baada ya klabu yake kuanza vibaya msimu na kushindwa kuwepo katika ligi ya mambingwa
Kocha wa Real Madrid Mourinho amekuwa akiripotiwa kumpeleka Bernabeu lakini bado kuna shaka shaka ya kuelekea huko na huku taarifa zaidi zikisema huenda akaenda kwa wapinzani wao jiji la Madrid hao si wengine bali ni Atletico Madrid.
Carlos Tevez kuvua unahodha Man City
Roberto Mancini anaelekea kumvua unahodha mshambuliaji wake Carlos Tevez
Taarifa zinaarifu kuwa ijumaa mchana katika uwanja wao wa mazoezi huko Carrington kulikuwa na mjadala mkubwa wa kuijadili ombi la mshambuliaji huyo la kutaka kuihama klabu yake hiyo.
City inajipanga kukutana dhidi ya Everton hapo kesho huku Mancini akitarajia kumpa kitambaa cha unahodha arm band ama mlinzi raia wa Ivory Coast Kolo Toure au Vincent Kompany.
Bado meneja huyo hajaweka wazi juu ya maamuzi yake hayo lakini maafisa wa juu wa klabu hiyo wanaamini kuna uwezekano mkubwa kwa unahodha ukamuangukia Toure.
Kumbuka kuwa mlinzi huyo huko nyuma chini ya Mark Hughes alishawahi kuwa nahodha na baadaye nafasi yake kuchukuliwa na Tevez majira ya kiangazi kwa lengo la kumbakisha Muargentina huyo huko Eastlands.
No comments:
Post a Comment