KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, February 3, 2011

Nyota mpya wa Reds Andy Carroll azungumzia kuondoka Fernando Torres

Mshambuliaji mpya wa Liverpool Andy Carroll amesema hana wasiwasi kuziba pengo la nyota wa zamani na kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo Fernando Torres.
Torres alikuwa ni kipenzi cha mashabiki wa Liverpool kabla ya kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho uliovunja rekodi nchini uingereza kwa pauni milioni £50 kuelekea Chelsea mwanzoni mwa wiki hii.
Carroll alijiunga na timu hiyo akitokea Newcastle kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni £35 muda mfupi mara baada ya Torres kuondoka huku mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akisema kuwa atafanya kile ambacho kimempeleka Anfield.
Akikaririwa anasema
"Torres alikuwa ni mchezaji mkubwa lakini nahitaji kuelekeza mawazo yangu katika mchezo , kujituma na kucheza kadri ya uwezo wangu,"
Carroll amekuwa ni mchezaji ghali wa uingereza katika historia ya uhamisho akitokea St James' Park kuelekea Anfield huku akishika nafasi ya tisa katika historia ya kandanda Duniani.
"ni kiasi kikubwa cha pesa lakini natakiwa kufanya jitihada ili nilingane na thamani ya pesa hiyo,"
"nimekuja kwa ajili ya kufunga mabao na kutengeneza nafasi kwa timu na ndicho kitu nitakachokifanya.


Mlinda mlango wa Arsenal Lukasz Fabianski nje msimu mzima
Mlindamlango wa Arsenal Lukasz Fabianski atakuwa nje ya uwanja kwa msimu uliosalia kutokana na kukubwa na maumivu ya bega.
Mlindamlango huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Poland mchezo wa mwisho kuidakia Arsenal ni ule dhidi ya Manchester City uliomalizika kwa suluhu ya 0-0 mchezo ambao ulifanyika January 5.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger akikaririwa anasema
"tumepata taarifa mbaya kuhusiana na Fabianski kwa sababu anahitaji kufanyiwa upasuaji wa bega.
"Fabianski ameamua kufanyiwa upasuaji huo baada ya kukutana na wataalamu kadhaa na upasuaji huo unatarajiwa kufanyika nchini Ujeruamni na hii inamaanisha atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia."

Fabianski amekuwa ni mlindamlango nambari moja wa klabu hiyo katika msimu huu akichukua nafasi hiyo kwa Manuel Almunia aliyekuwa akisumbulia na matatizo ya kifundo cha mguu mwezi septemba mwaka jana.


Man City inahitaji kubadilika kiakili Roberto Mancini
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema kikosi chake kinahitaji kubadilika kiakili baada ya kushuhudia hapo jana timu yake ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Birmingham City.
City haijashinda katika michezo yao mitatu iliyopita ikiwa na tofauti ya point nane dhidi ya wanaoongoza katika ligi kuu ya kandanda nchini uingereza Manchester United na huku matumaini ya kutwaa taji yakionekana kupungua.
Akikaririwa Mancini anasema
"tunahitaji kubadilika . tunapaswa tucheze mpira kwa mara nyingine na ndani ya wiki mbili tutakuwa tumesahau yote,"
"tunapaswa kubadilika kiakili , tunahitaji kujituma katika mazoezi."


Mlinzi wa Manchester United Gary Neville aachana na soka
Mlinzi wa Manchester United Gary Neville ameatangaza rasmi kuachana na soka la kulipwa.
Neville ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 35 ameichezea United michezo 602 mwaka 1992 na kufanikiwa kushinda mataji 85 akiwa na klabu hiyo.
Akikaririwa anasema
"nimekuwa mshabiki mkubwa wa Manchester United katika maisha yangu na kutimiza ndoto zote nilizokuwa nazo,"
"nasikitika siku zangu za kucheza zimefika mwisho . licha ya kwamba hilo litakuja kwetu sote na kwa upande wangu huu ndiyo wakati wake"
Mlinzi huyo wa kulia alijiunga United mwezi Julay mwaka 1991 kabla ya kuondoka mwezi September mwaka 1992 katika mchezo dhidi ya Torpedo ya Moscow ukiwa ni mchezo wa michuano ya UEFA.

Kwa kipindi hicho Gary ndiye aliyekuwa mlinzi bora wa kulia.
Meneja wa United Sir Alex Ferguson alikuwa ni sehemu ya mafanikio ya mlinzi huyo wakiwepo David Beckham, Nicky Butt, Ryan Giggs na Paul Scholes ambao walifanikisha kushinda taji la FA kwa vijana huo ulikuwa ni mwaka 1992.
Pamoja na wachezaji hao Neville alikuwa ni mchezaji anayepewa nafasi ya kwanza Old Trafford na kufanikisha kushinda taji la klabu bingwa barani ulaya, mataji nane ya ligi kuu ,mataji matatu ya FA na mataji mawili ya carling akiwa United.
Neville alichaguliwa kuwa nahodha wa United mwaka 2005 pia alikuwa ni mlinzi bora wa kulia wa uingereza chini ya makocha watano tofauti.

No comments:

Post a Comment