KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, February 2, 2011


Wenger akandia usajili wa Blues



Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amehoji uhalali wa Chelsea na kukosoa the Blues kutumia mapesa mengi katika kipindi cha uhamisho cha mwezi January huku tayari kukiwa na uzinduzi shirikisho la kandanda barani ulaya UEFA wa kuanza kudhibiti matumizi.
Wakati Wenger akionekana kutokuwa tayari kuingia ndani zaidi katika mambo ya soko la uhamisho wa wachezaji pia ameonekana kushtushwa na mpango wa Roman Abramovich kutumia pauni milioni £71.3 kufanya usajili wa wachezaji wawili Fernando Torres na David Luiz toka katika vilabu vya Liverpool na Benfica.
Mmiliki huyo raia wa Russian ameelezewa kufanya hivyo katika jitihada zake za kuipiga tafu Chelsea kuzindua mpango wa kuwania taji la Premier League lakini Wenger anaamini kuwa baada ya kuunga mkono utaratibu wa UEFA basi ni wazi kuwa “the Blues” itakuwa imejiweka katika hali ya kujifanya kuwa waumini wa mpango wa UEFA jambo ambalo si kweli.
Anakaririwa wenger akisema
"Chelsea iliunga mkono mapango wa UEFA wa kudhibiti matumizi lakini jambo la ajabu ni kwamba asubuhi yake imetangaza kupata hasara ya pauni milioni £70 na mchana wake wananunua wachezaji kwa tahamni ya pauni milioni £75m . logic iko wapi katika hilo?" anahoji Wenger.
"ni ngumu kudhania . Officially wamepigia kura “financial fair play” lakini hivi ni kweli wanaweza kutoa maelezo kwa namna gani wamefanya hivyo zaidi yangu."
Uefa imevionya vilabu baada ya siku ya mwisho ya uhamisho kukamilika
Uefa imevikumbusha vilabu kuwa mpango wake mpya wa udhibiti wa matumizi “new financial regulations” utazingatiwa baada ya kuwepo na kuvunjwa kwa rekodi za uhamisho wa wachezaji katika dirisha dogo la usajili la mwezi januari.
Sheria hiyo mpya ianatarajiwa kuingia katika utaratibu kuanzia msimu wa 2012 mpaka 2013 ikiwa na maana kuwa timu mbalimbali katika ulaya lazima zisimame ndani ya kipindi cha miaka mitatu , mean teams in European competitions must break even over a rolling three-year period
Vilabu ambavyo vimekuwa katika matumizi makubwa vitaruhusiwa kuonyesha hasara kuanzia pauni milioni £39m ndani ya kipindi cha misimu mitatu.
Vilabu vya uingereza pekee katika usajili wa mwezi januari vimefanya matumizi ya pauni milioni £225.
Jumatatu Chelsea na Liverpool pekee vimetumia nusu ya kiasi hicho cha pesa za uhamisho .

Chelsea “The Blues” ikivunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza kwa kulipa ada ya pauni milioni £50m kwa ajili ya kudaka saini ya mshambuliaji wa Liverpool Fernando Torres ilhali wekundu wa Liverpool wakitumia pauni milioni £35m kudaka saini ya mshambuliaji wa Newcastle Andy Carroll.
Liverpool ikatumia tena pauni milioni £22.7 kumsajili Mruguay Luis Suarez toka Ajax na Chelsea wakiilipa Benfica pauni milioni £21.3 kwa ajili ya kudaka saini ya mlinzi raia wa Brazil David Luiz.
Lakini hata hivyo matumizi makubwa hayo ya pesa yameibia maswali ya wadau kama vilabu hivyo vitaweza kukabiliana na mpango mpya wa udhibiti wa matumizi wa UEFA.
Jumatatu Chelsea ilitangaza hasara ya jumla ya pauni milioni £70.9 kwa mwaka uliomalizikia 30 June 2010 ikiwa ni zaidi ya pauni milioni £26.5 kwa mwaka uliotangulia.

Katika hatua nyingine klabu zinafikiria kupunguza hasara zao katika mwaka ujao.
Katika hilo wamepunguza utaratibu wa bonus na wameanza kufikiria mipango ya udhamini pamoja na kuangalia kupata zaidi kupitia ligi ya mabingwa na haki za luninga za ligi kuu pamoja na kuongeza bei za tiketi.
Hasara pia zitapunguzwa zaidi kwa klabu kukamilisha mauzo ya haki ya jina la klabu kule Stamford Bridge, jambo ambalo linaangaliwa huenda likaongeza uwezo wa kipesa kwa zaidi ya pauni milioni £10m kwa mwaka.
Hata hivyo inaangaliwa kuwa kwakuwa usajili wa Torres na Luiz ni wa miaka mitano na nusu katika mkataba basi inaangaliwa kuwa kiasi cha pauni milioni £75 haitakuwa tatizo kukabiliana na mapango wa UEFA wa udhibiti matumizi na hasara.
Lakini kwakuwa bodi ya utawala ya soka la ulaya inatarajia kuanza kusimamia mpango wake mwaka 2014 inaonekana kuwa vilabu vitaanza kuchukua hatua ya kukabiliana na hilo na kuweka uzani sawa wa matumizi katika vitabu vyao.

Wengi wamekuwa wakipigia kelele juu ya vilabu hivyo kufanya matumizi ya kufru akiwemo makamu wa rais wa AC Milan Adriano Galliani yeye amesema hiyo ilikuwa ni matumizi ya kichaa kwa akina Torres na Carroll.
Anakaririwa Galliani akisema
“Kila mtu anazungumzia juu ya kuanza kuweka mizani sawa katika vitabu lakini hawa wanafanya matumizi kama vichaa".
Fernando Torres kuonekana dimbani dhidi ya Liverpool
Carlo Ancelotti emekaririwa akisema mchezaji wake aliyevunja rekodi ya usajili ya Uingereza ya pauni £50 Fernando Torres anatarajiwa kuwepo dimbani katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani ya Liverpool jumapili hii
Anakaririwa akisema
"tutamjaribu kesho tomorrow na siku nyingine kama atakuwa hana tatizo anaweza kucheza dhidi ya liverpool," .
Ancelotti emeongeza hana kigugumizi juu ya kumtumia Torres pembeni yake Nicolas Anelka ambaye alifunga katika mchezo dhidi ya Sunderland sambamba na Didier Drogba.

Sturridge anasema future yake ni Chelsea
Mshambuliaji wa Chelsea Daniel Sturridge ana matumaini kuwa anaweza bado kutumia nguvu katika kujaribu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea kule Stamford Bridge licha ya kuwasili katika dakika za mwisho kwa Fernando Torres.
Sturridge mwenye umri wa miaka 21 pia amekazia juu ya uhamisho wa mkopo wa mwezi januari baada ya kujisajili na Bolton mpaka kumalizika kwa msimu na mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City atakuwa na kazi kubwa ya kufanya atakapo rejea Stamford bridge kwani atakuwa na kazi ya kusaka nafasi mbele ya wakali kama Torres, Didier Drogba, Nicolas Anelka na Salamon Kalou

Wayne Rooney anadhani Chelsea itakuwa ni changamoto kwa Man United
Nyota wa Manchester United Wayne Rooney anasema Chelsea inaweza ikaisukuma mbali timu yake katika kuwania taji la ligi hiyo.
Chelsea wako nyuma kwa points 10 kwa vinara wa ligi hiyo United huku wakiwa wameshinda michezo yao mitatu ya mwisho na wakiwa wamefanya usajili wenye gharama ya pauni milioni £70 na kuwadaka Fernando Torres na David Luiz.
Anakaririwa Rooney akisema
"bila shaka hatuja wafuta Chelsea mbali," said Rooney, who scored twice in Tuesday's 3-1 win over Aston Villa.
Mabingwa watetezi Chelsea wamesha poteza michezo sita ya ligi hiyo msimu huu na kuaonekana kama wamepoteza matumaini ya kuwania ubingwa kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya katika jumla ya michezo tisa.

Lakini bado “the Blues” wanaonekana kubadilika baada ya kufanikiwa kupata ushindi katika michezo kadhaa ikiwa ni pamoja na michezo dhidi ya Blackburn, Bolton na Sunderland,na inaweza kuwa katika mwendo mzuri kufuatia ukweli kuwa itakuwa na michezo miwili ya kukutana wao kwa wao yaani dhidi ya nyumbani na ugenini
Pamoja na hilo Rooney ana matumaini ushindi mara mbili dhidi ya Aston Villa utakuwa ni mwanzo mzuri wa kuanza kujiimarisha katika kupiga mabao.

Julio Cesar ajidhatiti Inter
Mlinda malngo nambari moja wa Inter Milan Julio Cesar amesisitiza kuwa atasalia katika kujidhatiti zaidi kwa mabingwa hao wa kandanda wa nchini Italia licha ya kuwepo na taarifa za tetesi kuwa amekuwa akitakiwa na mashetani wekundu Manchester United.
Mlinda mlango wa sasa tegemezi wa United Edwin Van der Sar anatarajiwa kujiweka pembeni katika majira ya kiangazi huku taarifa zikisema huenda akasajiliwa mlinda mlando wa Bologna Emiliano Viviano mwishoni mwa msimu huku Cesar akihusishwana kutaka kuondoka San Siro.
Wakati hayo yakiwa mlinda mlango huyo mwenyew umri wa miaka 31 raia wa brazil ambaye amekuwa katika kipindi kigumu cha mamumivu anasema atasalia Inter mpaka mkataba wake kumalizika

Christopher Samba ameanguka saini mpya na Blackburn Rovers
Mlinzi wa kati wa Blackburn Christopher Samba ameingia mkataba mwingine na klabu yake hiyo maktaba ambao utamuweka hapo Ewood Park mpaka 2015.
Samba amenukuliwa December akisema alikuwa akitafuta njia ya kuondoka lakini bosi wa Rovers Steve Kean ameonyesha kiu yake ya kuona mkongo huyo mwenyew umri wa miaka 26 akisalia hapo.

Wenger amtetea Fabregas dhidi ya madai ya Moyes
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amemtetea kiungo wake Cesc Fabregas baada ya meneja wa Everton David Moyes kudai kuwa nahodha huyo wa Gunners alipaswa kutolewa nje ya dimba wakati wa mapumziko.
Toffees walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 wakati wa mapumziko baada ya bao la utata la Louis Saha ambaye alionekana kama alikuwa ameotea.
Lakini baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 kule Emirates Moyes alikaririwa akisema
"maneno aliyotoa Fabregas kwa mawamuzi wa akiba na mwamuzi wa mchezo wakati wa mapumziko yalitosha kumtoa nje ya uwanja."
Wenger alilazimika kujibu kwa kusema
“Fabregas hakusema jambo lolote kwa mwamuzi katika muda huo wa mapumziko."

Hali ya mambo ilikuwa tofauti kwa pande zote mbili hususani baada ya bao la Saha alilofunga katika dakika ya 24 akiwa katika eneo ambalo mameneja wote wameonekana kukubali kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

No comments:

Post a Comment