KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 3, 2011

Hakuna mchezo wa marudiano kati ya Wladimir Klitschko dhidi ya Haye anasema meneja wa Klitscho Meneja wa bingwa wa pambano la mchezo wa masumbwi Wladimir Klitschko aliyemchapa David Haye amesema hakutakuwa na pambano la marudiano kati ya wawili hao lakini amesema uwezekano wa pambano la kaka yake Wladimir huyu ni Vitali Klitschko dhidi ya David haye linawezekana
Katika pambano la hapo jana usiku la uzito wa juu David Haye alipigwa kwa points pambano lililopigwa huko nchini Ujerumani katika uwanja wa Imtech au maarufu kama Imtech Arena.
Akikaririwa meneja huyo Bernd Bionte amesema "hakuna nafasi nyingine ya pambano la marudiano".
"Wladimir sasa anasonga mbele . Vitali ameonyesha nia ya kumpiga kwa knock-out Haye ."



Katika hatua nyingine amesema Wladimir alikuwa katika mpango wa kuzipiga dhidi ya bingwa Uingereza wa michuano ya jumuiya ya madola kati ya Tyson Fury na Dereck Chisora mchezo ambao unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Wembley au Wembley Arena mwezi huu.
"An interesting future opponent for him could be the winner of that fight," said the manager.
Mara kadhaa pambano la Klitschko dhidi ya Chisora limekuwa likiahirishwa kwa zaidi ya miezi minane sasa.
Katika hatua ngingine Promoter Frank Warren anaamini kuwa David Haye anapaswa kustaafu baada ya kushindwa katika pambano la hapo jana dhidi ya Wladimir Klitschko kwa points.
Majaji wote watatu walionekana kumpa nafasi Klitschko katika hesabu.
Akizungumza promoter huyo amesema "I think he should retire,".
Anaendelea kwa kusema "tayari amepata pesa ziko banki kuna haja gani ya kuendelea kutaka kupigana wakati hakuwa na sifa ya kushinda katika uzito unaostahili ?alikuwa katika uzito mzuri wa “cruiserweight” lakini hakuwa katika kiwango cha “heavyweight”"

Endapo Haye ataachana na masumbwi atasalia na rekodi ya mapambano 25 ya ushindi akishinda mapambano 23 kwa KO na kupoteza mawili.
Mwanamasumbwi huyo toka London aliingia katika masumbwi ya uzito wa juu kwa mara ya kwanza mwaka 2008 ambapo aliaanza kuzichapa dhidi ya Monte Barrett na kushinda kabla ya kumchapa Nikolai Valuev wa Russia na baadaye kutwaa taji la WBA na kuwa mwingereza wa kwanza kufanya hivyo baada ya Mwingereza mwingine Lennox Lewis kutwaa taji la uzito huo la dunia.
Mwenyewe anasema apewe muda wa kufanya maamuzi magumu ya kustaafu .

No comments:

Post a Comment