Manchester United imeongeza wigo
wa pointi hadi tano dhidi ya Manchester City kileleni mwa Ligi Kuu ya
Kandanda ya England lakin i ushindi wao dhidi ya Aston Villa uligubikwa
kwa mara nyingine na penalti iliyoonekana ni ya utata.
Ashley Young, ambaye alifanikiwa
kupata penalti wakati Manchester United walipocheza na QPR, kwa mara
nyingine alifanikiwa kupata penalti baada ya kutegewa na Ciaran Clark.
Kuguswa huko kwa Young kulikuwa kudogo sana
lakini Wayne Rooney alifanikiwa kufunga mkwaju huo wa penalti kabla
Danny Welbeck kuipatia Manchester United bao la pili.
Villa iliimarika kidogo baada ya kipindi cha
pili lakini walikuwa Rooney na Nani walioandika mabao mengine mawili
yaliyohitimisha karamu ya mabao 4-0.
Manchester United walionekana kikosi bora zaidi
katika kipindi cha kwanza na ushindi huo umepunguza pia deni la mabao ya
kufunga na Manchester City na sasa kuwa manne.
Lakini bado swali litaendelea kubakia kwa
wapenzi wa kandanda juu ya Young anavyojiangusha na aliposhutumiwa
alipofanya hivyo dhidi ya QPR, ambapo Shaun Derry aliadhibiwa kwa
kumsukuma mshambuliaji huyo wa pembeni na alioneshwa kadi nyekundu.
Rufaa iliyokatwa na Rangers ilitupiliwa mbali na
Chama cha Kandanda cha England na shutuma zitaendelea kumuandama Young
kutokana na alivyofanya kwa mara nyingine.
Na kubwa zaidi Young alifanya hivyo kwa timu
aliyowahi kuichezea na itaongeza zaidi chumvi kwenye jeraha kwa timu ya
Aston Villa.
Villa walishindwa kuivunja rekodi dhidi yao
wanapopambana na Manchester United, ambapo wamewahi kushinda mara moja
tu katika mechi 31.
Jambo muhimu ni kwamba wapo pointi sita juu ya
msatari wa kuteremka daraja na sasa wanajiandaa kwa pambano dhidi ya
Sunderland, Bolton na West Brom ambapo lazima watafute pointi
kujihakikishia hawateremki daraja.
No comments:
Post a Comment