KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 25, 2012

Busquets na Xavi: Tutamzuia Ronaldo


Wachezaji ngwinji wa mabingwa watetezi wa ulaya Hispania Busquets na Xavi wamesema wanayo dawa ya kumzima mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo katika mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Ulaya utakao pigwa jumatano.
Roja watakutana na Seleccao wakati ambapo Sergio Busquets na Xavi wakiamini kuwa wanajua mbinu ya kupunguza makali ya Cristiano Ronaldo katika mchezo huo.
Ronaldo alifunga goli zuri la kichwa lililoifungisha virago jamhuri ya Czech Republic kwenye robo fainali na kuwasogeza Seleccao kwenye nusu fainali.
Wakati wakali hao wa Barcelona wakiwa na hadhari kubwa kwa Ronaldo pia wanamatumaini wana uwezo wao binafsi wa kumpoteza mshambuliaji huyo wa Real Madrid man.
  Busquets amenukuliwa na gazeti la Marca akisema
"si kama ni mchezo baina ya Barcelona na Madrid ni Hispania dhidi ya Ureno na sote tunajua ukubwa wa uchezaji wa Cristiano.
"atakuwa mara zote anapumuliwa na na Alvaro Arbeloa na Alvaro anamjua vizuri kuliko mtu yoyote wote wanachezea Real Madrid. Lakini kumnyima nafasi ya kucheza mchezaji kama huyu inahitajika timu nzima kushirikiana."
Xavi anaamini yeye na wenzake wa sehemu ya ulinzi wataziba nafasi ya kucheza mchezaji huyu wa zamani bora wa dunia kufanya vitu vyake.
"tunapaswa kuwa tayari."anasema Xavi.
 "tutajaribu kuzuia pia kumnyima raha Cristiano na kumnyima nafasi hata ya kugeuka."
  Cesc Fabrigas :Hispania dhidi ya Ureno kama Clasico
Cesc Fabregas ana ulinganisha mchezo wa Hispania dhidi ya Ureno wa nusu fainali ya Euro 2012 kuwa kama Clasico kati ya Barcelona na Real Madrid.
Hispania imeelekea katika nusu fainali katika hali ya kujaribu kutete taji lao lakini huenda ikakutana na jaribio zito la kufanya hivyo dhidi ya shughuli pevu ya Ureno itakayo ongozwa na Cristiano Ronaldo.
Fabregas ameielezea Ureno kama hatari zaidi katika eneo la ushambuliaji na wachezaji karibu wengi toka kila upande wakitoka katika vilabu viwili pinzani nchini Hispania Barca na Real itakuwa kama ni El Clasico.
Fabrigas anasema
"Ureno ni moja kati ya timu ngumu, wanalinda vizuri na hatari katika kushambulia, ni kama ilivyo Real Madrid na tupaswa kuwa katika kiwango katika mchezo huo.
 “unaweza fananisha Real Madrid dhidi ya Barcelona katika mazingira ya aina ya uchezaji wa timu.
 “lakini kuna wachezaji tofauti na sisi pia tunawachezaji kutoka timu nyingi kwa hiyo haitakuwa sawa”
 

No comments:

Post a Comment