Release No. 094
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 15, 2012
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA)
KUJAZA NAFASI ZILIZO WAZI
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka
kuwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi
za Kamati ya Utendaji unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya
YANGA.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea kutoka Kamati ya Uchaguzi ya
YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA pamoja na nakala za
vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama sehemu ya taarifa ya awali ya
mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini
kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala za vyeti vya
kuhudhuria masomo ya sekondari (Secondary School Leaving Certificate) badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya sekondari (Certificate of Secondary Education).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya
YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama
wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote kujaza Fomu Na.1
ya maombi ya uongozi na kuambatanisha nakala ya cheti cha Elimu ya
Sekondari (Certificate of Secondary Education) kama
ilivyoainishwa kwenye Fomu Na.1 kipengere Na.9. Kamati ya Uchaguzi ya
TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA iwashauri wagombea ambao vyeti
vyao vimepotea wawasiliane na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
kwa maandishi ili kupata ‘Statement of Examination Results’ itakayotumwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kupitia TFF kuthibitisha kuwa wamehitimu elimu ya kidato cha nne.
Uhakiki wa vyeti vya elimu ya sekondari vya waombaji uongozi
hufanywa na NECTA na vyuo husika kwa elimu ya juu kwa chaguzi za
wanachama wa TFF. Wanachama wote wa TFF wanatakiwa kuzingatia kikamilifu
matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
Imetolewa na:
IDARA YA HABARI
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Kumbuka ni Mohamed Mbaraka peke yake ambaye ameshindwa kuwasilisha vyeti vyake na ambaye kimsingi alishatangaza kujiengua katika kinyanganyiro cha uchaguzi ndani ya klabu ya Yanga.
No comments:
Post a Comment