Yusufu Manji anayewania nafasi ya mwenyekiti katika klabu ya Yanga |
Pingamizi la
mwanachama wa klabu ya Yanga Abeid Abeid maarufu kama Falcon la kumwapinga wagombea wote wa
klabu hiyo limepingwa vikali na wazee wa klabu hiyo wakiongozwa na katibu wa
baraza la wazee mzee Ibrahim Akilimali
Wakizungumza
na waandishi wa habari hii leo wazee wameonyeshwa kushangazwa na pingamizi
la Falcon ambaye katika siku za nyuma alikuwa ni kiongozi ndani ya Yanga na
alikuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake katika
makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Mzee Ibrahim Akilimali akisisitiza jambo |
Falkon
katika pingamizi lake ameelezea sababu kuu tatu za kuweka pingamizi lake. Kwanza ni kuwa katiba ya Yanga si halala, pili haitambui kamati ya uchaguzi ya Yanga na pia anawapinga wagombea wote wanaowania nafasi za uongozi ndani ya klabu hiyo.
Wazee wa Yanga baada ya kusikia juu sababu za pingamizi la Abeid Falcon wameonyesha kushangaa kutokana na ukweli kwamba Falcon aliingia katika uwanachama ndani ya klabu hiyo mwaka 2007 klabu ikiwa chini ya katiba hii ya sasa lakini pia aligombea uongozi na kuchaguliwa kuwa mweka hazina mwaka 2007 kwa kupitia katiba hiyo iweje leo Falcon aipinge katiba iliyompa uongozi huko nyuma.
Wamesema kimsingi hawaingilii shughuli za kamati ya uchaguzi ya Yanga bali ni kujaribu kufafanua kile kilichomo ndani ya pingamizi hilo la mwanachama huyo.
Aidha wameendelea kuonyesha mshangao wao kwa Falcon kwani mwaka 2010 aligombea uongozi tena akiwania nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo kabla ya kungushwa na aliyekuwa mwenyekiti Loyd Nchunga na vipi aweke pingamizi juu ya katiba ambayo ilimpa uhalali wa kugombea uongozi.
Makao makuu ya klabu ya Yanga |
Wazee hao wameingiwa shaka huenda Falcon anatumiwa na watu fulani katika kujaribu kuuchafua uchaguzi huo mdogo wa klabu hiyo kongwe ambao unafuatia kujiondoa kwa idadi kubwa ya wajumbe wa kamati ya utendaji iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Loyd Nchunga mbaye naye alijiondoa katika uongozi baada ya shinikizo kubwa la wanachama wa klabu hiyo.
katika kuonyesha hasira zao zaidi baraza la wazee limeutaka uongozi mpya utakao chaguliwa katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 15 julay kumfuta uanachama Adeid Adeid"Falcom" ili kuinusuru klabu hiyo na watu ambao wamewaita ni wachochezi na wanaoshawishiwa kuvuruga utulivu ndani ya klabu hiyo kama Falcon aliyewahi kwenda mahakamani mwaka 2008 kupinga uongozi ulikuwa ukiongozwa na Imani Madega na katibu wake Lukas Kisasa.
No comments:
Post a Comment