KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 22, 2012

Ancelotti: ni juu ya Nene kuamua juu hatma yake PSG


Carlo Ancelotti anamatumaini kuwa Nene ataendelea kuwepo Paris Saint-Germain lakini ni juu ya mchezaji huyo mwenyewe kuamua hatma yake.
Uwepo wa winga huyo PSG upo mashakani tangu kuwasili kwa Ezequiel Lavezzi toka Napoli, na Nene amekuwa akifikiria nini aamue kuhusu offer ya  Corinthians.
Amenukuliwa Ancelotti na Eurosport akisema
"ni juu yake mwenyewe kuamua kama anataka kuondoka au anataka kusalia hapa kama atatuliza akili atapata maamuzi.
"nimeongea naye na klabu iko wazi tunachukua muda wetu kabla ya kuzungumzia juu ya kuongeza muda wa mkataba wake.
"tutakuwa wenye furaha kama ataamua kusalia kwa kuwa ni fantastic player na anaweza kuwa muhimu katika msimu ujao."
Nene mwenye umri wa miaka 31 alimaliza msimu katika ligi ya Ufaransa akiwa ni miongoni mwa wafungaji bora akitupia nyavuni jumla ya mabao 21.Maktaba wake PSG utamalizika kiangazi 2013.

No comments:

Post a Comment