KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 22, 2012

Ibrahimovic kujiunga na kikosi cha Paris Saint-Germain jumanne


 Bosi wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa Zlatan Ibrahimovic atafanya safari  kuelekea Marekani jumanne kujiunga na timu hiyo iliyoko katika ziara ya matayarisho ya msimu akiungana na wenzake wapya katika timu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden alikamilisha mipango yote ya uhamisho wake wenye thamani ya euro milioni 23 akitokea AC Milan tangu July 18 ikiwa ni siku nne baada ya mlinzi wa kibrazil Thiago Silva kufanya hivyo.
Mlinzi huyo wa kati hajaelekea katika ziara ya Marekani kwa kuwa yuko katika kikosi cha Mano Menezes ‘Selecao’ kinachojiandaa na Olympics lakini Ancelotti amesema Ibrahimovic ataungana nao jumanne huku taarifa nyingine zikiarifu kuwa atakuwepo nchini Ufaransa.

Kuelekea kwenye msimu mpya kocha huyo wa zamani wa Milan ana matumaini kuwa mswedesh huyo ataisaidia sana timu yake.
Mchezo wa kwanza wa kirafiki wa PSG ziarani Marekani utakuwa ni dhidi ya Chelsea utakao pigwa jumapili.

No comments:

Post a Comment