KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 22, 2012

Wenger ana imani ziara ya matayarisho ya ligi itaunganisha kikosi


 Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa ziara ya timu yake barani Asia itaongeza hari ya kikosi chake wakati huu ambapo klbu hiyo imeshabariki kuondoka kwa nahodha wake Robin van Persie.
Washika bunduki hao wameelekea Kuala Lumpur kucheza na Malaysian XI na baadaye kuelekea Hong Kong na Uchina kwa michezo mingine dhidi ya Manchester City na Kitchee SC.
Taarifa zinasema Van Persie amegomea safari hiyo kwa lengo la kuongeza nguvu mipango ya uhamisho wake kuelekea kwa mabingwa wa ligi kuu ya nchini uingereza.
Wenger pia amezungumzia juu ya madhumuni mengine ya ziara hiyo ya barani Asia kuwa ni kuungana na mashabiki wa soka timu hiyo ambao wako mashariki ya mbali.

No comments:

Post a Comment