KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 23, 2012

KAGAME CUP:JANGWANI SAFI,VIPI MSIMBAZI KESHO KWA WAUZA LAMBALAMBA WA AZAM.

Mfungaji wa bao la kusawazisha la Yanga Said Bahanuzi
(Picha Emmanuel Ndege)
Hatimaye mabingwa watetezi wa taji la michuano ya kombe Kagame Yanga ya Dar es Salaam imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya hii leo kufanikiwa kuitoa timu ngumu ya Mafunzo ya Zanziba kwa njia ya penati, kufuatia mchezo baina yao wa robo fainali kumaliza dakika tisini timu hizo zikienda sare ya bao 1-1.
Mafunzo walipata bao la uongozi katika kipindi cha kwanza likifungwa na Ally Othman Mmanga kwa kichwa baada ya kupokea mpira wa kona toka kwa Ally Juma Hassan.
Yanga walisawazisha bao hilo mapema katika kipindi cha pili kupitia kwa Said Bahanuzi kwa kichwa.
Dakika tisini zilimalizika timu hizo zikienda sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliingia katika hatua ya kupigiana penati ili kuamua nani wa kusonga mbele na ndipo mabingwa hao watetezi Yanga walipofanikiwa kupata penati zote tano kupitia kwa wapigaji Said Bahanuzi, Nadir Haroub Kanavaro,Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima na Athumani Iddi chuji.
Penati za Mafunzo zilizoingia wavuni zilipigwa na Salum Said Shebe ,Mohd Abdulrahim ,Jaku Juma Jaku huku Said Mussa Shaban akikosa penati ya pili .
Kiungo wa Yanga Chuji akiingia katika vyumba vya wachezaji pembeni ni Juma Abdul
(picha Emmanuel Ndege)
Kesho ni robo fainali ya tatu na ya nne ambapo Atletico ya Burundi inatarajiwa kukutana dhidi ya Vita Club katika robo fainali ya mapema saa nane mchana kabla ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba wakitarajiwa kukutana dhidi ya Azam FC saa kumi jioni.
mapema hii leo APR ya Rwanda imewafungisha virago  mabingwa wa soka wa Uganda URA baada ya kuwafunga kwa mabao 2-1 na sasa wanatarajiwa kukutana dhidi ya Yanga katika mchezo wa nusu fainali utakao pigwa jumatano.
Mabao ya APR yalifungwa na Jean Claude Iranzi na Selemani Ndikumana.


No comments:

Post a Comment