Cazorla mguu ndani mguu nje kwenda
Arsenal
Santi Cazorla |
Cazorla
mwenye umri wa miaka 27 alikuwa kwenye mipango ya Arsenal tangu msimu uliopita
lakini Malaga iligomea mpango huo tofauti na sasa ambapo kuna kila dalili za
klabu hiyo ya nchini Hispania kumtoa winga huyo licha ya kuendelea kuweka
pingamizi.
Winga huyo
ameripotiwa na gazeti la Guardian kuwa amefanya mazungumzo na Malaga na
kuwaeleza kuwa anatamani kuondoka na kuijulisha Arsenal kwamba angependa
kueleka kaskazini mwa London.
Mazungumzo
kati ya vilabu hivyo yanaarifiwa kufanyika katika Talks between the clubs are
reported to have taken place against a backdrop of increasing financial
Hali ya
sintofahamu imeingia katika klabu ya Malaga ambayo tayari taarifa zake zimesha
pelekwa katika chama cha wachezaji soka nchini Hispania (AFE) na wachezaji
wanne akiwemo Cazorla mwenyewe kuwa wamekuwa hawana mshahara.
Chini ya Under
sheria mpya ya iliyotolewa mwezi April, kklabu hiyo inatakiwa mpaka kufikia Julai
25 iwe imetoa majibu ya malalamiko hayo na mpaka kufikia mwisho wa mwezi kuwa
imefikia makubaliano na wachezaji wake juu ya tatizo hilo.
Kushindwa
kufanya hivyo kunaweza kunaweza kuwashusha daraja na kuondoshwa katika ligi ya
mabingwa.
Cazorla alijiunga
na Malaga akitokea Villarreal kwa uhamisho wa euro €19 majira ya kingazi
yaliyopita na baada ya msimu huu amekumbwa kadhia ya kukosa mshahara ikiwa ni
pamoja na bonas zake kiasi kutamka kutaka kuondoka.
Sneijder: Stramaccioni ndiye bora baada ya Mourinho
Stramaccioni |
Wesley Sneijder |
Wesley
Sneijder anaamini kuwa Andrea Stramaccioni ndiye mtu muafaka kuisaidia Inter kurejea
kileleni baada ya kuvurunda katika kampeni ya 2011-12.
kocha huyo
mwenye umri wa miaka 36 ameanguka saini ya kupiga kazi ya kufundisha kwa
mkataba wa kudumu kama kocha wa Nerazzuri majira haya ya
kiangazi baada ya aliyekuwa akifanya
kazi hiyo kwa mkataba wa muda mfupi baada ya Claudio Ranieri.
Sneijder ana
matumaini kuwa bosi huyo kijana ni mtu sahihi kwa kazi hiyo pale Inter baada ya
kuondoka kwa Jose Mourinho.
amenukuliwa
akisema
"Stramaccioni
ndiye bora kwa Inter baada ya Mourinho,".
"klabu
hii inajenga mustakabali wa baadaye na Stramaccioni ndiye kocha wa mpango huo
hapa Inter katika kipindi hiki. ana mpango mkubwa na timu hii"
Sneijder alikuwa
chini ya Mourinho katika miaka ya 2009 na 2010.
Alves: Barca ilinichanganya
Dani Alves |
Alves mwenye
umri wa miaka 29 alihusishwa na kutaka kuhamia katika klabu za Anzhi
Makhachkala na Manchester City mapema katika majira haya ya uhamisho wa
kiangazi lakini Barcelona haikuchukua hatua zozote za kukanusha habari hizo za
kuwepo mazungumzo ya yeye kweli kutaka kuondoka.
Mlinzi huyo
raia wa Brazil katika kipindi hicho alikuwa akidhani kuwa klabu yake maarufu
kama Blaugrana
ingekanusha taarifa uvumi huo.
amenukuliwa
akisema
"ni
kweli kulikuwepo uvumi kuwa sitakuwepo Barca
na nilichanganyikiwa na klabu yangu haikuingilia kati,"
"hata hivyo
naona niko juu ya hilo na kama wakati utawadia na kama klabu yangu itakuwa
hainihitaji tena nitakubaliana na hilo na nitaondoka kama ilivyokuwa wakati najiunga
nayo."
Alves
alijiunga na Barcelona kwa ada ya kushitua ya euro milioni €35.5 mwaka 2008 baada
ya kutoa huduma katika klabu ya Sevilla ambayo ilishinda mataji mawili ya UEFA
Cup , na Copa del Rey.
Maamuzi ya Hoffenheim kumuacha Babel ni kinyume cha mkataba
Ryan Babel |
Kitendo cha kuondoka kwa Ryan Babel toka katika klabu ya Hoffenheim kimeelezwa kuwa kimekwenda kinyume na taratibu za kimkataba kwa mduchi huyo. Kauli hiyo imetolewa na wakala wa mchezaji huyo.
Kocha Markus
Babbel amenukuliwa akisema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 pamoja na
Edson Braafheid wanaweza kuondoka Rhein Neckar Arena na kumkosoa zaidi
mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool kwa kiwango kibovu alicho onyesha
tangu ajiunge na klabu hiyo January 2011.
Hata hivyo
wakala wake Babel , Winnie Haatrecht, amesisitiza kuwa sababu zinazo tolewa na Hoffenheim
kumruhusu mshambuliaji huyo kuondoka na mbaya kabisa kumfukuza mpaka kambini ni
kinyume mambo yaliyomo ndani ya mkataba.
Amenukuliwa
Haatrecht akiongea na De Telegraaf akisema
"katika
kipindi cha uhamisho wa dirisha dogo tuliingia katika makubaliano ya kimkataba
na Hoffenheim. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na mshahara wa Ryan kuongezwa
mara mbili endapo atacheza michezo angalau michezo minne msimu ujao"
"jambo
la kushangaza ni kuwa , Hoffenheim imemuondosha katika orodha yao wakati ambapo
bado ana mwaka mmoja katika mkataba wake.
"leo
hii , Ryan wanataka afanye mazoezi na kikosi cha kiba, inabidi asubiri. haitakuwa
rahisi kwake kupata uhamisho, kwasababu Hoffenheim haitaki hata kuwepo na
uhamisho wa mkopo.
Yanga-Mbiwa anafikiria juu ya hatma yake ya baadaye
Mapou Yanga-Mbiwa |
AC Milan imekuwa
ikivutiwa na mlinzi huyo Yanga-Mbiwa mwenye umri wa miaka 23 ili kuziba nafasi
ya Thiago Silva, lakini Nicollin ameonya
"Yanga-Mbiwa hataondoka” .
"ili
kuwa na makubaliano zaidi na Milan, tungehitaji kuwa na makubaliano zaidi. Hatuna makubaliano hivyo hakuna makubaliano ya
kueleweka.
"najua
kuwa wametoa offer ya euro milioni €6 lakini hata kama wataongeza mara tatu
ya hiyo bado haitoshi na mbaya zaidi sina mbadala wake, kwa hiyo ni wazi kuwa
hataondoka. Haijalishi hata kama yuko ukingoni mwa mkataba wake."
Lakini
wakati hayo yakiendelea mchezaji mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa kuna
uwezekano mkubwa wa kuondoka majira haya ya uhamisho wa kiangazi.
No comments:
Post a Comment