KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 24, 2012

KAGAME CUP:MASIKINI SIMBA NDO BASI TENA.

Mabao matatu ya John Boko yametosha kuiondosha mabingwa wa soka Tanzania bara katika michuano ya kombe la Kagame katika mchezo wa leo wa robo fainali uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya bao 3-1 Simba walionekana kuwa katika kiwango kibovu tofauti na ilivyo dhaniwa kabla ya mchezo huku ikipata bao lake kupitia kwa Shomari Kapombe.
Matokeo hayo sasa yanaifanya Azam kucheza na Vita Club ya Congo DRC baada ya timu hiyo kuifunga Atletico ya Burundi kwa mabao 2-1katika mchezo wa mapema mchana.
Simba imekuwa ikilalamikiwa kukosa kiungo kizuri tangu kuanza kwa michuano hii iliwatumia ikiwatumia Mwinyi Kazimoto na Haruna Moshi lakini walionekana kudhibitiwa na wachezaji wa kiungo wa Azam ambao walidhibiti vema sehemu hiyo wakiongozwa na Ibrahim Mwaipopo na Ramadhani Chombo.

Mashabiki wa Azam wakishangilia timu yao dhidi ya Simba
Katika mchezo kati ya Vita Club dhidi ya Atletico ya Burundi, bao la Basilwa Bakola katika dakika ya 93 liliimaliza ndoto za warundi kusonga mbele.Bao lakwanza la Vita liliwekwa kimiani na Etekiama Taddy ambaye anaonekana kuelekea kuwa mfungaji bora wa mashindani haya baada ya bao lake la dakika ya saba kumfanya afikishe jumla ya mabao sita akifuatiwa na Said Bahanuzi wa Yanga mwenye magoli matano.
Bao la Atletico lilifungwa na Pierre Kwizera.

No comments:

Post a Comment