KAGAME CUP:Mshike mshike na maandalizi ya nusu fainali.
|
Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame |
|
Azam fc mazoezini Chamazi |
|
APR FC ya Rwanda |
|
Vita Club ya DRC
Mashindano
ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati almaarufu Kombe la Kagame
2012, yamefikia hatua ya Nusu Fainali ambapo timu nne(4) zitachuana siku ya
alhamis kusaka timu timu mbili ambazo zitacheza fainali siku ya jumamosi katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabingwa
watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans itashuka dimbani kucheza na tim
ya APR kutoka Rwanda katika nusu fainali ya pili itakayofanyika jioni majira ya
saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Nusu Fainali
ya kwanza itaanza majira ya saa 8:00 mchana kwa kuzikutanisha timu za Azam FC
(Tanzania) na timu ya AS Vita ya (DRC), timu ya Azam imefanikiwa kuingia hatua
ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya Simba SC ya Tanzania pia kwa jumla ya
mabao 3-1.
AS Vita nayo
imefanikiwa kufika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya
Atletico FC ya nchini Burundi kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochzwa hapo awali.
Young
Africans iimefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya
Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-3, kufuatia kumalizika kwa dakika
90, ztimu zote zikiwa sare ya mabao 1-1.
APR kutoka
Rwanda iliifinga timu ya URA kutok Uganda mabao 2-0 katika mchezo wa robo
fainali na hivyo kupata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.
Kocha mkuu
wa Young Africans Tom Saintfiet akiongea na tovuti ya klabu
wwww.youngafricans.co.tz alisema anajua mchezo dhidi ya APR ni mgumu, kwani
mchezo wa kwanza walishinda kwa mabao 2-0, hivyo anaamini APR wataingia
Uwanjani wakiwa na nia ya kusaka ushindi ili waweze kucheza hatua ya fainali.
Saintfiet
pia alisema pamoja na kuwa na mchezo huo mgumu dhidi ya APR, anaamin vijana
wake wako katika hali nzuri ya ushindi, na maandalizi yote ya mchezo
yamekamilika, hivyo anaamini timu yake Young Africans itaibuka na ushindi
katika mchezo huo.
|
No comments:
Post a Comment