KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 30, 2012

HII NI FURSA YA KUONA MAANDALIZI YA BONDIA WA TANZANIA SELEMANI KIDUNDA KABLA YA KUVAANA NA VASILII BELOUS WA MOLDOVA KATIKA MASHINDANO YA LONDON YA OLYMPIC.



Katika michezo sita ya awali ya uzito wa Welterweight (69kg) ya michezo ya Olympic bondia mzoefu na mwenye uwezo wa hali ya juu toka nchini  Moldovan Vasilii Belous alikutana dhidi ya mtanzania  Selemani Kidunda.
Tangu kupigwa kwa kengele bondia huyo alionekana kumfikia vilivyo bondia Mtanzania Kidunda na kisha kuanza kufululiza straight one-twos na hatimaye akamshinda Kidunda kwa points 20 kwa saba7.
Akiongea na Rockersports toka nchini Uingereza kunako fanyika michezo hiyo ya Olympic, Kidunda amesema kimsingi amekubali kushindwa lakini huo ni mchezo na kuna kushinda na kushindwa hivyo mashabiki wake wasikate tama.
Hata hivyo nilipomuuliza sababu za kushindwa na Vasilii Belous amesema kikubwa ni kwamba mpinzani wake alikuwa akitumia mbinu chafu ya kumshika kila mara katika round mbili za mwanzo jambo ambalo lilimfanya mwamuzi kumkanya kila mara hata hivyo alifanikiwa kumdhibiti katika round ya tatu nay a mwisho.
Mchezo huo ulikuwa ni wa round tatu na hivyo ukamalizika kwa Kidunda kupigwa kwa points 20 kwa 7.
Sasa Belous anasubiri mzunguko wa pili dhidi ya bondia toka  Ukraine Taras Shelestyuk.points 4 katika round tatu alikuwa anaonyenywa

No comments:

Post a Comment