Meneja wa Arsenal Arsene Wenger:
Giroud na Podolski hawatakuwa tayari kwa ajili ya msimu mpya.
Arsene
Wenger amekiri kwamba maandalizi ya Arsenal kwa ajili ya msimu mpya
hayajakwenda kama alivyopanga baada ya kudai kuwa Lukas Podolski na Olivier
Giroud hawatakuwa tayari kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya kandanda ya
England.
The Gunners wamemaliza
ziara katika Bara la Asia kwa kucheza na mabingwa wa ligi kuu ya Hong Kong Kitchee hapo jana na kutoka sare ya mabao 2-2 lakini
mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa
juma umehairishwa na kuifanya sasa kusaliwa na mchezo mmoja tu dhidi ya Koln.
Mapema wiki
hii Wenger ameweka wazi kwamba Jack Wilshere hatarejea hadi Octoba mwaka huu na
kueleza kwamba wachezaji wake wengi huenda wasiwe tayari mwanzoni mwa msimu mpya
wakiwa wamesalia majumbani kwao wakati wa ziara.
Amesema
wachezaji ambao hawakuwepo katika ziara hiyo watahitaji michezo ya kutosha
lakini baadhi watahitaji mchezo mmoja.
Tottenham inaamini Adebayor hatakamilisha
mipango ya kurudi Manchester City
Tottenham bado
inamatumaini ya kukamilisha mpango wa kumsaini kwa pauni milioni £5 mshambuliaji
wa zamani wa Asernal Emmanuel Adebayor,licha ya mshambuliaji huyo kurejea
katika mazoezi katika kikosi cha vijana cha Manchester City jumatano.
Mazungumzo baina
ya Adebayor na Spurs kwasasa yamekuwa yakiendelea na atakuwa akifanya mazoezi
katika kituo cha mazoezi cha Manchester City cha Carrington wakati ambapo
kikosi cha wakubwa kikiendelea na ziara ya Austria, Malaysia na China.
Spurs ilikuwa
na matumaini ya kukamilisha uhamisho wa Adebayor wakati wakiwa zirani nchini
Marekani mwishoni mwa wiki hii lakini hata hivyo mambo yanaonekana kwenda
kinyume na matarajio.
Manchester
City na Spurs zilifikia makubaliano wiki mbili zilizo pita kutoa ada ya pauni
milioni £5 kwa ajili ya mchezaji huyo kufuatia kuwepo kwa mkopo muda mrefu White
Hart Lane lakini Adebayor akikataa kutokana na kutoafikiana juu ya maslahi yake
binafsi ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la London.
Lakini hata
hivyo kuna matumaini kuwa mpango huo utafanikiwa kutokana na utashi wa meneja mpya
wa Spurs Andre Villas-Boas kutaka kujenga safu yake ya ushambuliaji lakini pia
mwenyewe Adebayor kutaka mkataba wa kudumu ndani ya klabu hiyo.
Taarifa
zinasema kuwa Adebayor amerejea kufanya mazoezi cha City akiwa na Roque Santa
Cruz ambapo wamekuwa wakipata mshahara wa pauni £280,000 kwa wiki"
Imefahamika
kuwa safari ya mshambuliaji huyo kuelekea White Hart Lane haitakamilishwa mpaka
mapema mwezi ujao.
Adebayor alikuwa
akiichezea Spurs akiwa mchezaji muhimu kwa mkopo msimu uliopita chini ya Harry
Redknapp ambayo aliifungia jumla ya mabao 17 katika ligi kuu na kutoa pasi za
mwisho zilizo zaa mabao 11 katika jumla ya michezo 33 aliyochezea timu hiyo.
Mshambuliaji
huyo raia wa Togo alijiunga na City akitokea Asernal kwa ada ya uhamisho ya
pauni milioni £25 mwaka 2009, lakini
alijikuta akikosa nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya mchezo dhidi ya Red
Bull Salzburg mchezo wa michuano ya Europa December 2010.
Galliani: Matokeo ya hivi karibuni
yamedhihirisha AC Milan kuendelea kuwa moto
Mkurugenzi
wa AC Milan Adriano Galliani anaamini kuwa mchezo mzuri ulionyeshwa na timu yao
katika michezo ya maandalizi ya kuanza kwa msimu imedhihirisha kuwa kocha Massimiliano Allegri amekimiliki vema kikosi
imara cha timu hiyo.
Kuuzwa kwa Zlatan
Ibrahimovic na Thiago Silva kuelekea Paris Saint-Germain, lakini pia kuwasili kwa
mchezaji mwenye kiwango cha juu Riccardo Montolivo, kunaleta faraja na
matumaini kuwa Rossoneri itatwaa taji.
Aidha Galliani
ametoa maoni yake juu ya michezo ya wiki iliyopita ambapo walipata ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Chelsea na Schalke kuwa
imepigia mstari juu ya ubora wa Milan.
Baadhi ya
mashabiki wa Milan bado wana matumaini kuwa klabu hiyo bado itakuwa na cheche
zake licha ya kuacha wachezaji wao kadhaa waliokuwa nyota na wazoefu huku Galliani,
akinukuliwa akisema timu hiyo kigogo nchini Italia kwasasa haina nafasi ya
kufanya uwekezaji kwa wachezaji wenye majina makubwa.
Milan ambayo
ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Juventus msimu uliopita katika ligi
ngumu ya Serie A inatarajia kuanza kampeni ya taji katika msimu mpya wa 2012-13 dhidi ya Sampdoria August 26.
No comments:
Post a Comment