Uruguay imekuwa ndio taifa la mwisho kukamilisha nafasi ya kucheza kombe la dunia 2014 nchini Brazil baada ya kwenda suluhu 0-0 katika mchezo wa pili wa marudiano wa mtoano dhidi ya Jordan.
Uruguay ilikuwa katika nafasi nzuri zaidi hata kabla ya mchezo huo wa jana kufuatia matokeo mazuri ya mchezo wa mkondo wa kwanza ya ushindi wa mabao 5-0.
"tunafuraha wote kwasababu ukweli ni kwamba ilikuwa ni safari ndefu" amesema mshambuliaji Edinson Cavani.
TIMU ZILIZOFUZU
Africa: Algeria, Cameroon, Ghana, Ivory Coast, NigeriaAsia: Australia, Iran, Japan, South Korea
Europe: Belgium, Bosnia-Hercegovina, Croatia, England, France, Germany, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, Switzerland, Spain
North & Central America & Caribbean: Costa Rica, Honduras, Mexico, United States
South America: Argentina, Brazil (hosts), Colombia, Ecuador, Chile, Uruguay.
Taifa hilo kutoka Amerika ya kusini kwasasa liko katika nafasi ya sita kwa ubora wa viwango vya FIFA na inakumbukumbu ya kutwaa taji miaka ya 1930 na 1950 and na kufanikiwa kufika nufu fainali mwaka 2000 nchini Afrika kusini.
Kikosi cha kocha Oscar Tabarez kilimaliza katika nafasi ya tano katika vita ya kufuzu kutoka katika mabara na kushindwa na Ecuador kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga
No comments:
Post a Comment